Ayatollah Sayyid Mujtaba Husseini, mjumbe wa Baraza la wataalamu wa uongozi, katika mazungumzo yake na Shirika la Habari la Hawza alitilia mkazo jukumu la Mwezi wa Ramadhani katika kuimarisha diplomasia ya kiroho na kitamaduni, na kusema kwamba; Kufunga katika Ulimwengu mzima wa Kiislamu kunaimarisha hisia za umoja na upendo kati ya mataifa ya Kiislamu.
Mwanachama wa Baraza la wataalamu wa uongozi alisema kuwa; Uratibu wa kitamaduni na kidini katika mwezi wa Ramadhani unaweza kuimarisha uhusiano kati ya nchi za kiislamu na kuongeza kusema: "Ikiwa tutaliona suala la diplomasia kuwa ni uhusiano kati ya serikali tu, Mwezi wa Ramadhani huenda usilete athari ya moja kwa moja, lakini ikiwa tutaipanua maana ya diplomasia na kuielekeza kwenye uhusiano kati ya mataifa na uhusiaabo kati ya jamii za Kiislamu, basi Mwezi wa Ramadhani utakuwa na nafasi muhimu kama athari ya kiroho inayowaunganisha," Kufunga katika Ulimwengu wa Kiislamu ni chanzo cha hisia za mshikamano na ushirikiano kati ya mataifa, na hili huongeza upendo na ushirikiano miongoni mwa waislamu.
Aliongezea kwa kusema: "Katika Mwezi wa Ramadhani, ratiba za kidini na kitamaduni zinazofanyika katika nchi mbalimbali, iwapo zitasambazwa kwa njia ya vyombo vya habari, zitazalisha hisia za umoja na kujivunia kuwa sehemu ya jamii kubwa ya waislamu inayozidi bilioni moja au mbili, uhusiano huu wa kiroho utaimarisha upendo na heshima kwa dini na Mwezi wa Ramadhani utajulikanwa kama alama ya umoja kati ya Waislamu Duniani."
Ayatollah Husseini akizungumzia jukumu la serikali alisema: "Kama vile baadhi ya nchi hushirikiana kuhusu sherehe za Mwaka mpya na kuimarisha tukio hili kama alama ya kitamaduni, Mwezi wa Ramadhani pia unaweza kuwa fursa ya kuanzisha uhusiano wa karibu zaidi kati ya nchi za Kiislamu, Serikali zinaweza kushirikiana na kubadilishana mipango ya kidini na kitamaduni katika Mwezi wa Ramadhani ili kuimarisha mshikamano miongoni mwa mataifa ya kiislamu."
Maoni yako