Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Makarem Shirazi amezungumzia suala la "Jinsi Hazrat Mahdi (a.t.f.s) alivyotangamana na Watu wa Kitabu" kwa Kwa mujibu wa shirika la habari la Hozha, Ayatullah Makarem Shirazi alizungumzia suala la "Jinsi Hazrat Mahdi (AS) alivyotangamana na Watu wa Kitabu" kwa maandiko yafuatayo ambapo alisema:
Kwa mujibu wa baadhi ya riwaya, Hadhrat Mahdi (a.t.f.s) atatawala baina ya watu wa Taurati kwa mujibu wa Taurati yao, baina ya watu wa Biblia kwa mujibu wa Biblia zao, na baina ya watu wa Zaburi kwa mujibu wa zaburi zao.
Maswali mawili yanazushwa hapa: Swali la kwanza ni je, atabaki yeyote katika Ahlul-Kitab (Watu wa Kitabu) baada ya kuja kwa Imam al-Zaman (Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake na faraja yake ).
Na swali la pili ni je, nini maana ya kutawala baina ya watu wa kitabu (Ahlul Kitab) kwa mujibu wa Kitabu chao cha Mbinguni?
Kwa kujibu swali la kwanza, tunasema:
Watu wote hawatasilimu wakati wa Utawala wa Imam al-Zaman (a.t.f.s), na kuna watu kutoka katika Watu wa Kitabu ambao hawakuwa dhidi yake na hawatataka kufanya mgogoro wowote na kupigana dhidi yake na Serikali yake.
Kundi hili la Watu wa Kitabu wanaweza kuwa chini ya wajibu wa Uislamu na Waislamu na kuendelea na maisha yao kwa kutoa jizya.
Lakini kuhusu swali la pili, kuna uwezekano wa aina mbili:
1. Makusudio, ni kuvifananisha vitabu hivi (vya Mbinguni) na sehemu (maalum) iliyotoa amri (kwao) ya kuingia katika Uislamu na kumwamini Mtume Mtukufu (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na Aali zake). Mambo yale yaliyomo katika nakala za Biblia ambayo yamo mikononi mwa Hadhrat Mahdi (a.t.f.s) au Hadhrat Isa (amani iwe juu yake), na mambo yale yale yanayotimiza hoja na uthibitisho kwa Watu wa Kitabu.
2. Makusudio, ni kwamba Hadhrat Imam Mahdi (a.t.f.s) atatoa Hukumu za Vitabu hivi juu ya wale wafuasi wa Vitabu hivyo (wanaoviamini na kuvifuata) ambao hawajasilimu bado; Lakini wanaisho kwa kutekelezwa dhima na wajibu wa Uislamu.
Maoni yako