Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Hadhrat Ayatollah Al-Udhma Sayyid Musa Shubairi Zanjani katika hotuba yake alitaja riwaya ya ushauri wa Hadhrat Imam Ridha (amani iwe juu yake) kuhusu siku za mwisho za Mwezi wa Sha'ban, ambapo alisema:
Soma sana dua hii katika muda uliosalia wa Mwezi wa Sha'ban:
«اَللّهُمَّ اِنْ لَمْ تَکُنْ غَفَرْتَ لَنا فیما مَضی مِنْ شَعْبانَ فَاغْفِرْ لَنا فیما بَقِیَ مِنْهُ»
Ewe Mwenyezi Mungu! Ikiwa haujatusamehe hadi sasa katika sehemu iliyopita katika Mwezi huu, basi tusamehe katika sehemu iliyobakia ya Mwezi huu!.
Ni kweli kwamba Mwenyezi Mungu huwakomboa waja wengi kwa kuwakweka mbali na Moto wa Jahanamu katika Mwezi huu (wa Sha'ban).
Wasail al-Shia, Juzuu ya 10, uk wa 302.
Maoni yako