Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Jawadi Amuli ametoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Ayatullah Wahid Khorasani (Mwenyezi Mungu amrehemu).
Ifuatayo ni nakala ya ujumbe wake:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.
Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na hakika kwake Yeye tutarejea.
Kufariki Marji' mwenye hadhi ya juu, Ayatullah Al-Udhma Wahid Khorasani (Mwenyezi Mungu aitakase roho yake), ni msiba mkubwa na tukio chungu katika historia.
Tunatoa salamu za rambirambi kufuatia msiba huu mkubwa kwa Wali Al-Asr (roho zetu ziwe fidia kwake), Maraji' wa kidini wa ulimwengu wa Kiislamu, Hawza za kielimu na Umma wa Kiislamu unaofungamana na Wilaya, hususan watoto wa Maraji' huyo, ambao ni miongoni mwa walimu mashuhuri katika elimu ya Fiqhi.
Vilevile, tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu amnyanyulie daraja Faqihi huyo aliyetangulia mbele ya haki, na aijalie familia yake tukufu subira njema katika kukabiliana na msiba huu mkubwa.
Jawadi Amuli
Maoni yako