Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, ifuatayo ndiyo matini ya ujumbe wa rambirambi wa Ayatullah Sayyid Hashem Husseini Bushehri kufuatia kifo cha Ayatullah Wahid Khorasani (Mwenyezi Mungu amrehemu):
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.
Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na hakika Kwake Yeye tutarejea.
Kufariki mwanachuoni mchamungu, faqihi mwenye upeo mkubwa wa elimu na Marji' mkuu wa ulimwengu wa Kishia, Ayatullah Al-Udhma Wahid Khorasani (Mwenyezi Mungu autakase moyo wake), kumesababisha huzuni na majonzi makubwa katika Hawza, jamii, waumini na wafuasi wa madhehebu ya Ahlul-Bayt (as).
Faqihi huyo mtukufu na Marji' mwenye busara alitumia maisha yake yenye baraka katika njia ya kueneza mafundisho yenye nuru ya Uislamu, kulinda utukufu na mipaka ya madhehebu ya Shia, kulea na kuwaandaa wanafunzi, pamoja na kueneza elimu za Ahlul-Bayt (amani iwe juu yao). Kazi zake za kielimu na kiroho zitabaki kuwa hazina yenye thamani kubwa kwa Hawza za kielimu na ulimwengu wa Kishia.
Bila shaka, kumpoteza mwanachuoni huyu mashuhuri katika nyanja za elimu na kiroho ni pigo kubwa kwa Hawza za kielimu na ulimwengu wa Kiislamu. Jina na kumbukumbu za marehemu huyo mtukufu zitabaki milele katika kumbukumbu za kielimu na kidini za Hawza na ulimwengu wa Kishia.
Mimi binafsi ninatoa salamu za rambirambi kutokana na msiba huu mzito na wenye kuumiza moyo kwa Mtukufu Baqiyyatullah Al-A'dham (roho zetu ziwe fidia ya udongo wa nyayo zake); kwa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu (Mwenyezi Mungu aendeleze kivuli cha uongozi wake); kwa Maraji' wakuu wa kuigwa (Mwenyezi Mungu aendeleze baraka zao); kwa wanazuoni wakuu wa dini; kwa Hawza za kielimu; kwa wanafunzi wake; kwa wafuasi na wenye kumpenda; pamoja na familia tukufu ya marehemu, hususan wanawe watukufu.
Aidha, ninamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu amnyanyue marehemu huyo mwanachuoni mchamungu katika daraja za juu kabisa na amfufue pamoja na Mawalii Wake. Pia, ninamuomba Mwenyezi Mungu awajalie jamaa wa marehemu na wote waliofiwa subira njema na malipo makubwa.
Sayyid Hashem Husseini Bushehri
Maoni yako