Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Nouri Hamadani ametoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Faqihi, Ayatullah Wahid Khorasani (Mwenyezi Mungu amrehemu).
Ifuatayo ni nakala kamili ya ujumbe wake:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.
Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na hakika kwake Yeye tutarejea.
Kufariki Faqihi mashuhuri na mwenye hadhi ya juu, Ayatullah Sheikh Haji Hussein Wahid Khorasani (Mwenyezi Mungu amrehemu), kumesababisha huzuni na masikitiko makubwa.
Mwanachuoni huyo mkubwa, kwa kunufaika na mafundisho ya wanazuoni mashuhuri wa Hawza za Khorasan na Najaf, alifikia daraja ya juu kabisa katika elimu ya Fiqhi. Aidha, wanafunzi wengi walinufaika na chemchemi ya elimu yake yenye manufaa makubwa.
Kutumia muda wa karne nzima kutetea heshima na utukufu wa Ahlul-Bayt (amani iwe juu yao), pamoja na kueneza utamaduni wa Maimamu watoharifu (as) kupitia majukwaa ya mihadhara na ufundishaji, lilikuwa miongoni mwa sifa za kipekee za mwanachuoni huyo aliyekuwa akiyatekeleza kwa vitendo yale aliyoyafundisha.
Bila shaka, kufariki Faqihi huyu mtukufu kutakuwa ni hasara isiyoweza kufidiwa kwa Hawza za kielimu.
Mimi binafsi, ninatoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Marji' huyu mwenye hadhi ya juu, kwa Mtukufu Baqiyyatullah Al-A'dham (Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake), Hawza za kielimu, watoto wake waheshimiwa na wanazuoni, hususan Ayatullah Sheikh Haji Sadiq Larijani, pamoja na wapenzi na wafuasi wake wote.
Ninamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu amjaalie marehemu huyo mwema daraja za juu kabisa na makazi mema huko Akhera.
26 Aban 1405 Hijria Shamsia (17 Novemba 2026)
Hussein Nouri Hamadani
Maoni yako