Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza,, Ayatullah Makarim Shirazi ametoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Ayatullah Wahid Khorasani (Mwenyezi Mungu amrehemu), ambaye alikuwa miongoni mwa Maraji' wakubwa wa Taqalidi.
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.
Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na hakika kwake Yeye tutarejea.
Taarifa ya kufariki kwa Faqihi mwenye hekima na uelewa wa kina, Ayatullah Haji Sheikh Hussein Wahid Khorasani (Mwenyezi Mungu autakase udongo wa kaburi lake), imesababisha huzuni na masikitiko makubwa.
Mwanachuoni huyo wa kimungu alitumia maisha yake yenye baraka katika kutetea njia ya Wilaya na madhehebu ya Ahlul-Bayt (amani iwe juu yao), pamoja na kuwaongoza waumini. Aidha, katika kufufua na kuhuisha mafundisho na mambo yanayohusiana na Watukufu hao, hususan katika kutetea mafundisho ya Fatimiyyah na Alawiyyah, hakusita kufanya juhudi zozote.
Darsa zake zenye manufaa makubwa, idadi kubwa ya wanafunzi waliolelewa na kufundishwa katika darasa la Faqihi huyo mcha Mungu, pamoja na vitabu na maandiko mbalimbali alivyoviandika, ni miongoni mwa urithi wa kudumu ulioachwa na maisha yake ya kielimu. Hakika, Hawza za kielimu ya Qom, Najaf na Khorasan zitaendelea kunufaika na matunda ya urithi huo.
Mimi binafsi, ninatoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Faqihi huyo mchamungu na mwenye mapenzi makubwa kwa Mtukufu Wali Al-Asr (roho zetu ziwe fidia kwake), Hawza za kielimu, familia tukufu ya marehemu pamoja na watoto wake waheshimiwa.
Ninamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu amnyanyulie marehemu huyo mwema daraja za juu kabisa na amfufue pamoja na Mawalii wa Mwenyezi Mungu. Vilevile, ninamuomba Mwenyezi Mungu awajalie ndugu na jamaa zake waliobaki subira njema na malipo makubwa.
Na amani, rehema na baraka za Mwenyezi Mungu ziwe juu yenu.
Qom – Nasser Makarim Shirazi
Maoni yako