Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, kwa kutegemea maelezo ya Amal al-Maakhidhi, Makamu Mwenyekiti wa Shirika la Insan la Haki na Uhuru, mashambulizi yanayoendelea kutekelezwa na Saudi Arabia nchini Yemen hayajaishia kwenye masoko na makazi ya watu pekee, bali yameenea hadi kwenye maeneo ya mahabusu.
Al-Maakhidhi alikumbushia mauaji yaliyotokea katika kituo kikuu cha mahabusu katika wilaya ya Al-Hazm, mkoani Al-Jawf, tarehe 16 Shahrivar 1405 kwa kalenda ya Hijria Shamsia, sawa na tarehe 7 Septemba 2026. Tukio hilo lilitokea wakati familia za wafungwa zilipokuwa zimekwenda kuwatembelea ndugu zao, na kusababisha kuuawa na kujeruhiwa makumi ya watu, wakiwemo wanawake na watoto waliokuwa wamekwenda kufanya ziara hiyo.
Katika mahojiano yake na tovuti ya Ansarullah, Al-Maakhidhi alisisitiza kwamba mashirika mengi ya ndani yanayojishughulisha na masuala ya haki za binadamu, yakiongozwa na Shirika la Insan, yamejitahidi kurekodi na kuweka kumbukumbu za uhalifu mwingi unaodaiwa kutekelezwa na adui wa Saudi Arabia nchini Yemen.
Alifafanua kwamba mashirika hayo yana jalada kamili la nyaraka na ushahidi, ambalo linaipa Yemen uwezo wa kuchukua hatua za kisheria dhidi ya adui wa Saudi Arabia na kumwajibisha kwa mujibu wa sheria. Kwa mujibu wa Al-Maakhidhi, mashirika ya haki za binadamu, katika kipindi cha sasa cha kuongezeka kwa mvutano nchini Yemen, yameandika mfululizo wa uhalifu mkubwa katika maeneo ya pwani ya magharibi na Taiz.
Alibainisha kwamba miongoni mwa matukio makubwa zaidi ni mauaji yaliyotokea katika soko la Mafraq Mawiyah, lililoko katika wilaya ya Al-Ta'ziyah, kusini mwa mkoa wa Taiz. Tukio hilo lilitokana na kushambuliwa soko hilo kwa ndege za kivita, na kusababisha kuuawa na kujeruhiwa raia kati ya 47 na 50.
Katika muktadha wa kurekodi ukiukaji wa haki za binadamu, Makamu Mwenyekiti wa Shirika la Insan la Haki na Uhuru, wakati wa kutangaza ripoti hiyo, alisisitiza kwamba ufuatiliaji uliofanywa ulihusu matukio 85 ya ukiukaji yaliyotokea katika kipindi cha kuanzia Januari 2018 hadi Septemba 2026.
Kati ya matukio hayo, 80 yalihusishwa na vikosi vya Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu. Ukiukaji huo unajumuisha mauaji, majeruhi, watu kupotezwa kwa nguvu, kukamatwa kiholela, kuhamishwa kwa lazima na kushambuliwa kwa wavuvi.
Maoni yako