Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, sambamba na kuongezeka hatua za utawala wa Kizayuni katika Quds inayokaliwa kwa mabavu, Msikiti wa Al-Aqsa unakabiliwa na vikwazo vinavyozidi kuongezeka pamoja na mashambulizi ya walowezi wenye misimamo mikali. Hatua hizo zimeambatana na maonyo kuhusu kulengwa sehemu ya mashariki ya msikiti huo na eneo linalouzunguka Mlango wa Bab al-Rahma.
Wasiwasi katika Quds inayokaliwa kwa mabavu umeongezeka kutokana na kuimarishwa hatua za wavamizi zinazolenga kubadilisha hali iliyopo katika Msikiti Mtukufu wa Al-Aqsa na kuondoa utambulisho wake wa Kiislamu. Mchakato huu umeambatana na kuongezeka mashambulizi, kuwekwa vikwazo dhidi ya waumini wanaokwenda kuswali na kutolewa amri za kuwapiga marufuku kuingia msikitini karibu wakazi 1,000 wa Quds. Wakati huohuo, maonyo yametolewa kuhusu kulengwa sehemu ya mashariki ya Msikiti wa Al-Aqsa na maeneo yanayozunguka Bab al-Rahma.
Hatua hizi zinaambatana na mfululizo wa vitendo vinavyofanywa katika viwanja vitakatifu vya Msikiti wa Al-Aqsa, vikiwemo kuendesha ibada na taratibu za Kitalmudi, kucheza dansi na kupiga makofi wakati wa mashambulizi yanayofanywa na walowezi wa Kizayuni wenye misimamo mikali.
Sambamba na hatua hizo, juhudi za kulazimisha hali mpya katika eneo hilo zinaendelea. Jambo hili limezidisha wasiwasi kuhusu kuendelezwa mipango ya kugawa Msikiti wa Al-Aqsa kwa misingi ya nyakati na maeneo, ili kuathiri namna eneo hilo takatifu linavyotumika.
Maoni yako