Jumapili 11 Oktoba 2026 - 15:20
Mkutano wa Kitaaluma kuhusu Palestina, Muqawama wa Kustahimili na Ulimwengu wenye Haki Zaidi Wafanyika Afrika Kusini

Mkutano wa kitaaluma wenye anuani ya “Palestina, Muqawama wa Kustahimili na Ulimwengu wenye Haki Zaidi” umefanyika katika kampasi ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al-Mustafa mjini Johannesburg, Afrika Kusini, ukiambatana na maadhimisho ya kumbukumbu ya mwaka wa operesheni ya Tufani ya Al-Aqsa.

Shirika la Habari la Hawza - Katika hatua ya kwanza ya utekelezaji wa vitendo wa makubaliano ya ushirikiano kati ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al-Mustafa, tawi la Afrika Kusini, na Taasisi ya Kitaifa ya Elimu ya Juu ya Afrika, mkutano huo ulifanyika Jumatano, tarehe 7 Oktoba 2026, mjini Johannesburg.

Mkutano huo ulijikita katika suala la Palestina, muqawama wa kutafuta haki na kutafakari urithi ulioachwa na mashahidi Sayyid Hassan Nasrullah, Ismail Haniyeh, Yahya Sinwar na Muhammad al-Deif. Aidha, ulitoa fursa ya majadiliano kuhusu vipengele vya kibinadamu, kimaadili, kisiasa na kijamii vinavyohusiana na suala hilo.

Wazungumzaji katika mkutano huo walikuwa Dkt. Sayyid Hamidreza Haqiqi, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al-Mustafa, tawi la Afrika Kusini; Bi. Nongoma Zulu, mhitimu wa shahada ya uzamili katika Sayansi ya Siasa kutoka Chuo Kikuu cha Johannesburg; Dkt. Juliet Aileen Joseph, profesa mkuu katika Chuo Kikuu cha Johannesburg; Dkt. Muhammad Hatji, profesa mshiriki katika Kituo cha Utafiti wa Masomo ya Kimataifa; Dkt. Mbekeni Nkosi, profesa mkuu katika Chuo Kikuu cha Wits; na Profesa Rasigan Maharaj, profesa wa Masuala ya Kiteknolojia katika Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Tshwane.

Mkutano huu wa pamoja ulikuwa mwanzo wa hatua ya utekelezaji wa ushirikiano kati ya Chuo Kikuu cha Al-Mustafa na Taasisi ya Kitaifa ya Elimu ya Juu ya Afrika. Kuandaliwa programu hiyo kwa kushirikisha wataalamu wa kitaaluma kulitoa fursa ya kuunganisha uwezo wa kielimu wa taasisi hizo mbili na masuala ya kibinadamu na kijamii, pamoja na kupanua majadiliano kuhusu haki na utu wa binadamu.

Utekelezaji wa programu hii unachukuliwa kuwa ishara ya kwanza ya vitendo ya makubaliano kati ya taasisi hizo mbili, na hatua muhimu katika njia ya kupanua ushirikiano wa pamoja katika nyanja za elimu, utamaduni na utafiti.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha