Jumapili 11 Oktoba 2026 - 18:50
Simulizi za Wayahudi Kuhusu Mwisho wa Utawala Wao Zinathibitisha Ahadi za Qur’ani

Hawza/ Mwenyekiti wa Umoja wa Kimataifa wa Wanazuoni wa Muqawama amesema kuwa; anasisitiza tena kwamba Wayahudi wote, wawe Wazayuni au wasiokuwa Wazayuni, wanaamini kuwa kuanguka utawala wao ni jambo lisiloepukika.

Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Maher Hamoud, Mwenyekiti wa Umoja wa Kimataifa wa Wanazuoni wa Muqawama, aliyasema hayo katika kikao kilichoitwa “Uthabiti na Uaminifu”, kilichofanyika katika ofisi yake mjini Sidon, kwa mnasaba wa kuadhimisha mwaka wa tatu tangu kuanza Operesheni ya Tufani ya Al-Aqsa.

Sheikh Hamoud alisema: “Tunarudia kusisitiza kwamba; Wayahudi wote, wawe Wazayuni au wasiokuwa Wazayuni, wanaamini kuwa kuanguka utawala wao ni jambo lisiloepukika, na wameukadiria utawala huo kudumu kwa miaka themanini. Jambo hili linaonekana wazi katika maandishi ya viongozi wao, kuanzia kwa Ben-Gurion, mwanzilishi wa utawala huo, hadi Ehud Barak.”

Aliongeza kusema: “Tunayaamini masimulizi ya Wayahudi kwa sababu yana mambo mahususi na ya kina, kwa mfano, vitabu vyao vinataja kwamba jeshi litakaloingia Lebanon litasimama katika kijiji cha Sultan Yaqub, kilichoko katikati ya eneo la Bonde la Biqaa, hiki ni kijiji kidogo ambacho watu wengi hawajui hata jina lake, lakini tukio hilo ndilo hasa lililotokea mwaka 1982. Kwa hiyo, Mwenyezi Mungu akipenda, masimulizi ya Wayahudi kuhusu jambo hili yatakuwa ya kweli, na yatazidisha yakini yetu kuhusu yale yaliyotajwa katika Qur’ani Tukufu na hadithi za Mtume (s.a.w.w.).”

Mwenyekiti huyo wa Umoja wa Wanazuoni wa Muqawama aliendelea kusema kwamba; ni muhimu kulaani vyombo vya habari vinavyoendelea kurudia madai kwamba muqawama ndio unayohusika na uharibifu wa maeneo ya kusini mwa Lebanon, kama vile vinavyodai kwamba muqawama ndio unayohusika na uharibifu wa Ghaza. Alieleza kuwa vyombo hivyo vinaonekana kutaka kuhalalisha uhalifu dhidi ya ubinadamu, uharibifu na mauaji ya kimbari yanayofanywa na Wazayuni.

Sheikh Hamoud aliendelea kusema kuwa; sifa ya kuwa na uhusiano wa kitaifa na Lebanon haipaswi kuhodhiwa na mtu au kundi lolote, slibainisha kuwa baadhi ya watu wanadai kwamba kuinga mkono Ghaza kunapingana na uzalendo wa Lebanon, ilhali madai hayo yanakinzana na misingi ya msingi kabisa ya ubinadamu na uzalendo wa Lebanon. Aidha, aliongeza kuwa; wanawakosoa wale wanaoadhimisha miaka mia moja tangu kuandikwa kwa Katiba ya Lebanon, lakini wakati huohuo wanasahau maandishi ya Michel Chiha, ambaye aliukosoa Uzayuni.

Sheikh Hamoud alieleza kuwa; Michel Chiha aliwahi kusisitiza kwamba iwapo utawala wa Wazayuni ungeanzishwa katika ardhi ya Palestina, Lebanon nayo isingeweza kuendelea kusimama imara. Sababu ni kwamba utawala wa Wazayuni umejengwa juu ya misingi ya ubaguzi wa rangi, ilhali Lebanon inaweza kudumisha uthabiti wake kupitia makubaliano na maelewano kati ya madhehebu yake mbalimbali.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha