Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Mu’min Al-Rifai, Mshauri wa Mahusiano ya Kidiplomasia nchini Lebanon, amesisitiza tena, kupitia taarifa yake, kujifunga na njia ya muqawama pamoja na kuhifadhi wosia. Aidha, katika maadhimisho ya mwaka wa tatu tangu kuanza Operesheni ya Tufani ya Al-Aqsa, amethibitisha tena msimamo wake wa kusimama pamoja na wananchi wa Palestina.
Sheikh Al-Rifai alieleza kuwa; alishiriki katika hafla ya kuadhimisha mwaka wa tatu wa Tufani ya Al-Aqsa, baada ya kualikwa na Darul-Iftaa ya Palestina nchini Lebanon na nje ya nchi, hafla hiyo iliandaliwa chini ya kaulimbiu isemayo: “Pamoja na Palestina, Tufani ya Heshima… Kuanzia Ghaza hadi Kusini mwa Lebanon.”
Alibainisha kuwa lengo la hafla hiyo lilikuwa kuifanya upya ahadi na kiapo cha uaminifu kwa jambo kuu na tukufu linalowaunganisha watu wenye heshima na wapigania uhuru duniani, nalo ni suala la Palestina katika nyanja zake zote: ardhi yake, wananchi wake, muqawama wake na wakimbizi wake.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na Hujjatul-Islam Sheikh Hassan Abdullah, aliyekuwa akiongoza ujumbe wa Jumuiya ya Wanazuoni wa Kiislamu nchini Lebanon, pamoja na ushiriki mkubwa wa marafiki na waungaji mkono wa Palestina kutoka nchini Lebanon na sehemu mbalimbali za dunia.
Maoni yako