Shirika la Habari la Hawza – Jumatatu, 5 Oktoba 2026, katika mji wa Napoli, Italia, wakati wa mkusanyiko wa kila wiki wa wanawake uitwao “Kwa ajili ya maisha huko Ghaza,” uliofanyika katika Mtaa wa Toledo, eneo la Largo Berlinguer, baadhi ya watalii wahuni wa Israel walikaribia eneo la mkusanyiko na, kwa matusi na lugha chafu, wakawashambulia wanawake waliokuwapo.
Mkusanyiko huu hufanyika kwa lengo la kuwakumbuka watoto walioathiriwa na mauaji ya kimbari, na katika kuunga mkono uhuru wa watu wa Palestina.
Wanawake waliokuwepo hawakusalimu amri mbele ya uchochezi huo, walisalia eneo la mkusanyiko na kwa kupaza sauti kaulimbiu, waliepuka kunaswa katika mtego wa uchochezi wao; wala hawakuwaruhusu wavamizi hao kujionyesha kuwa wao ndio waathirika kama ilivyo desturi yao.
Mara moja, vyombo vya usalama vilivyokuwepo eneo hilo vilielezwa kuhusu tukio hilo, Maafisa walipofika waliwataka watu hao wa Israel waliokuwa wakifanya fujo waondoke mahali hapo.
Hata hivyo, si tu kwamba walikataa kuondoka au kuwasilisha nyaraka walizoombwa na polisi, bali baada ya kuwatukana maafisa hao, waliwashambulia pia kimwili. Kufuatia mzozo huo, magari zaidi ya polisi yalitumwa eneo hilo ili kuwazuia.
Baadhi yao walifanikiwa kutoroka, lakini wengine walipelekwa kituo cha polisi—hatua iliyopokelewa kwa shangwe na raia wa Napoli waliokuwepo katika Mtaa wa Toledo uliokuwa na watu wengi.
Mfumo huo uko wazi: uchochezi wa mara kwa mara, kila mahali na bila heshima yoyote, unaoishia katika mashambulizi na mapigano, kwa dhana kwamba kana kwamba mtu anaweza kujiweka juu ya sheria na haki, bila kuwajibika mbele ya yeyote.
Maoni yako