Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri ilitangaza katika taarifa yake kwamba; walowezi hao wamefanya vitendo vya uchochezi na kutekeleza ibada za kidini za Kizayuni ndani ya eneo takatifu la Msikiti wa Al-Aqsa. Misri pia imeonya kuhusu kuendelea na kuongezeka vitendo kama hivyo, ikisema: Vitendo hivi vinafanyika sambamba na shughuli pana zaidi za ujenzi wa makazi ya walowezi pamoja na taarifa ambazo Cairo imezikataa.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri imeongeza kusema: Vitendo hivi vinaweza kufuatwa na kubadilishwa kwa mipangilio iliyopo na kulazimishwa hali mpya katika Msikiti wa Al-Aqsa. Cairo imetaka kuhifadhi hali ya kihistoria na kisheria ya eneo hili takatifu na maeneo matakatifu yaliyopo mjini Jerusalem, pamoja na kulinda hadhi ya kidini ya Msikiti wa Al-Aqsa.
Aidha, imetolewa tahadhari kwamba kurudiwa matukio haya kunaweza kuongeza kwa kiwango kikubwa hali ya mvutano na kutishia usalama na utulivu katika maeneo yote ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu pamoja na eneo zima.
Chanzo: Egypt Independent.
Maoni yako