Jumatano 7 Oktoba 2026 - 01:00
Vita Dhidi ya Matakatifu, Juhudi za Serikali ya Bahrain za Kuondoa Utambulisho wa Kidini katika Jamii ya Mashia

Hawza/ Waziri wa Mambo ya Ndani wa Bahrain ametishia kuongeza hatua dhidi ya Mashia wa nchi hiyo na kufanya suala la wanazuoni waliofungwa kuwa gumu zaidi.

Kwa mujibu wa ripoti ya idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, likinukuu “Mir’at Bahrain”, Rashid bin Abdullah, Waziri wa Vizuizi na Magereza (Waziri wa Mambo ya Ndani), kwa mara nyingine amedhamiria kuongeza hatua zake dhidi ya wanazuoni waliofungwa, ambao wamepelekwa nyuma ya nondo kwa tuhuma na dhuluma. Kisingizio chake kilichoandaliwa tayari ni “vita dhidi ya Wilayat al-Faqih”. Waziri huyo katika kauli zake za hivi karibuni amesema: “Wawakilishi wa Wilayat al-Faqih walijaribu kuitawala jamii ya Kishia nchini Bahrain na kupenya katika taasisi za Serikali na chombo cha kutunga sheria.”

Badala ya kutafuta njia ya kutoka katika mgogoro au kutatua matatizo yaliyopo nchini Bahrain (ambayo yalianza tangu kipindi cha vita dhidi ya Iran na ushirikiano wa utawala wa Bahrain pamoja nayo), Rashid bin Abdullah anaonekana akiwa na sera zenye kulipuka na zenye kuchochea mgawanyiko, ambazo inaonekana Serikali imekusudia kuzifikisha hadi mwisho.

Mapambano yasiyokoma dhidi ya wanazuoni na maulamaa waliofungwa hayatoi dalili ya kuelekea katika suluhisho; kwa sababu utawala unasisitiza kuendelea na hatua zake dhidi yao, na licha ya ukosoaji wote unaopinga uhalali wa kisheria na kiusalama wa kuwekwa kwao kizuizini, mfumo huo unaendelea na sera zake za dhuluma.

Baadhi wanaamini kuwa kauli za hivi karibuni za Rashid bin Abdullah ni ishara mbaya sana na wanatabiri kwamba, kutokana na uwezekano wa kutolewa hukumu nzito sana, suala la wanazuoni waliofungwa linaweza kukabiliwa na mabadiliko hatari. Suala hilo sasa limekuwa wazi: ni vita ya chuki dhidi ya imani halisi za kidini nchini. Kufanya shughuli za Kiislamu na za Kisharia za Madhehebu ya Shia kuwa kosa la jinai kumekuwa jambo kuu linaloishughulisha wizara hii; wizara ambayo maamuzi yake huchukuliwa chini ya uongozi wa mtawala mwenye mamlaka kamili nchini.

Waziri wa Vizuizi na Magereza anataka kutuma ujumbe wake unaojirudia, ambao Serikali haina uwezo wa kuutoa kwa namna nyingine: kuleta hofu na woga katika jamii na kuwatisha watu ili kuwaweka mbali na imani na itikadi zao, na huenda hata kujaribu kuwaweka mbali na itikadi ya [Wilayat al-Faqih], kiasi kwamba wasisikie tena jina la “Wilayat al-Faqih” katika mkusanyiko wowote, darsa ya kidini, msikiti, matamko ya maombolezo, au hata katika vikao vya kuomboleza na kuimba nyimbo za maombolezo.

Tunaposikia maneno ya Rashid bin Abdullah, hakuna kinachokuja akilini mwetu isipokuwa mifano ya fitina, kuupiga kwa nguvu muundo wa kijamii na kuondoa wingi uliopo miongoni mwa makundi mbalimbali ya watu. Juhudi za kuimarisha hali ya kujitenga na dhehebu la Kishia zinaendelea, kwa lengo la kuwafanya Mashia ambao Serikali itakuwa na udhibiti kamili juu ya Sheria, utambulisho na itikadi zao.
 
Lakini subiri! Kinachotokea baada ya kiwango hiki cha kuongezwa kwa hatua, ufuatiliaji na ukamataji dhidi ya wanazuoni, kinaonesha kiwango cha muqawama na kutosalimu amri kwa ujumla kwa wafuasi wa Ushia huu; watu ambao wanaona shughuli na utendaji wa wanazuoni kuwa ni mstari mwekundu ambao hawatajadiliana juu yake chini ya tishio lolote, hata liwe kubwa kiasi gani; kwa msingi wa kauli hii: “Ikiwa ni lazima sisi sote tufungwe, basi tufungeni wote; sisi hatutafanya maridhiano juu ya dini na itikadi yetu.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha