Jumatano 7 Oktoba 2026 - 00:30
Wote Walioamuru na Waliohusika Katika Kuuwawa Imam Shahidi, Wanastahili Hukumu ya Kuuwawa

Hawza/ Ayatullah Rajabi Katika Darsa ya Juu ya Usul amesema: Wote Walioamuru na Waliohusika Katika Kuuwawa Imam Shahidi, Wanastahili Hukumu ya Kuuwawa.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Mahmoud Rajabi, mwanzoni mwa kikao cha kwanza cha darsa ya Juu ya Usul katika mwaka wa masomo wa 1405 H.S, katika Taasisi ya Kielimu na Utafiti ya Imam Khomeini (ra) mjini Qom, huku akirejea kuuwawa kishahidi Ayatullah Sayyid Ali Khamenei (Mwenyezi Mungu amrehemu kwa rehema zake), alisema: Tunauanza mwaka mpya wa masomo tukiwa tumenyimwa uwepo wa kimwili wa msaidizi muhimu zaidi, mwenye kufungua njia na msaidizi wa kweli wa Hawza; mtu ambaye kuliko mtu mwingine yeyote aliijua vizuri Hawza, uwezo wake na mapungufu yake, na kuliko mtu mwingine yeyote alijua njia ya kutatua matatizo ya Hawza na kuifanya Hawza iendane na mahitaji ya zama, na pia tulishuhudia uungaji mkono kamili na wa moja kwa moja wa Hawza kutoka kwa mwanazuoni huyu mkubwa.

Mjumbe wa Baraza Kuu la Hawza nchini Iran aliongeza: Bila shaka, kuuwawa kwake kishahidi ilikuwa msiba mkubwa, lakini baraka za uwepo wake baada ya kuuwawa kishahidi na kutokana na kuuwawa kwake kishahidi zimekuwa nyingi sana na zisizo na mfano; na tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema hizi ambazo chini ya kivuli cha uwepo wake mtukufu, katika kipindi cha maisha yake yenye heshima na baada ya kuuwawa kwake kishahidi, zimewafikia wananchi wetu na mfumo wetu.

Nguvu ya Mfumo wa Kiislamu

Mkuu wa Taasisi ya Kielimu na Utafiti ya Imam Khomeini (ra), huku akirejea nguvu ya mfumo wa Kiislamu, alisisitiza: Leo, kwa baraka ya uwepo huu mtukufu, maadui wetu wakubwa zaidi ambao walikuwa wakifanya watakavyo duniani, yaani Wazayuni na utawala wa Marekani wenye kuchukiza, wako katika hali ya udhaifu ambayo haijawahi kuwa na mfano katika historia ya maisha yao machafu, na Jamhuri ya Kiislamu iko katika nafasi ya juu kabisa ya nguvu, na dola kubwa halisi yenye nguvu duniani leo ni mfumo huu mtukufu; hii ni neema kubwa sana.

Wananchi Wameonesha Uaminifu Wao

Mjumbe wa Kamati ya Uongozi ya Baraza la Wataalamu wa Uongozi aliendelea: Pamoja na nguvu ya mfumo wetu, pia tunao wananchi waaminifu, wanaofuata Wilaya, wenye subira, walio katika uwanja na wenye uelewa kamili; ambao kwa zaidi ya siku mia mbili walishiriki katika viwanja na kuonesha uaminifu wao kwa Wilaya, mfumo na nchi yao. Ushiriki huu wenye umoja ni mtukufu; umoja ambao hauna shaka yoyote ya kidunia ndani yake, na wote walikuja kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kwa ajili ya kuulinda mfumo, neema hizi kubwa na makumi ya mifano mingine ya neema hizi zote, ni miujiza ambayo tumepata kwa baraka ya damu ya kiongozi wetu shahidi.

Baraka za Uwepo wa Ayatullah Sayyid Mujtaba Husseini Khamenei (Mwenyezi Mungu Aendelee Kumhifadhi)

Mjumbe wa Baraza Kuu la Hawza nchini Iran, huku akirejea baraka za uwepo wa Ayatullah Sayyid Mujtaba Husseini Khamenei (Mwenyezi Mungu aendelee kumhifadhi), alisema: Moja ya baraka za kiongozi wetu shahidi ni uwepo wa mrithi wake mwema, ambaye katika mazingira magumu zaidi Mwenyezi Mungu amemjaalia kuwa miongoni mwa watu wetu na mfumo wetu, na anaendelea kuuongoza mfumo kwa nguvu zilezile, uimara uleule na miongozo ileile ya hekima; licha ya kutokuwepo kwake hadharani, kupitia ujumbe wake anaiongoza jamii kwa namna hii na anaendelea na njia ileile. Hii pia ni neema kubwa sana, na tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa ajili yake, na tunamuomba Mwenyezi Mungu kwamba mpaka kudhihiri kwa Hadhrat Baqiyyatullah (a.j.), kivuli cha mrithi huyu mwema wa kiongozi shahidi kiendelee kuwa juu yetu kwa heshima na nguvu.”

Wote Walioamuru na Waliohusika Katika Kuuwawa Imam Shahidi, Wanastahili Hukumu ya Kuuawa

Ayatullah Rajabi, katika sehemu ya mwisho ya hotuba yake, huku akisisitiza ulazima wa kulipiza kisasi kwa ajili ya kiongozi shahidi, alisema: Watu wote ambao walishiriki katika jinai hii ya kutisha na msiba huu mkubwa wanastahili hukumu ya kuuwawa, na kulipiza kisasi kwa ajili ya Imam shahidi ni matakwa ya wananchi wetu wote, bali ni matakwa ya Waislamu wote, kwa mujibu wa wajibu wao wa kisheria wa kidini, na pia ni matakwa ya watu wote wanaopenda uhuru duniani. Kauli hizi ambazo wakati mwingine baadhi ya watu huzitoa kinyume na mtazamo huu, bila shaka zinapingana na misingi ya kidini, misingi ya kiakili na kimataifa, na pia zinapingana na maslahi ya mfumo, nchi na wananchi wetu.

Tunawajibika mpaka kwa mtu wa mwisho ambaye alihusika katika msiba huu mkubwa na kuuawa kiongozi wetu shahidi na ambaye bado yuko hai; mpaka mtu wa mwisho kati yao, ni wajibu wetu kuhakikisha kwamba yeyote aliyehusika katika msiba huu mkubwa sehemu yoyote aliyopu duniani anapata adhabu inayostahili kutokana na matendo aliyoyafanya.

Ushiriki wa Wananchi Uendelee Kadiri Kiongozi Wetu Mpendwa Atakavyoona Inafaa

Mkuu wa Taasisi ya Kielimu na Utafiti ya Imam Khomeini (ra), mwishoni alisisitiza: Umoja huu mtukufu na ushiriki wa wananchi wa saa zote za mchana na usiku unapaswa pia, kadiri kiongozi wetu mpendwa atakavyoona inafaa, kuwa na hamasa zaidi na kuendelea.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha