Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza kutoka Tehran, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Ali Saeedi, Mkuu wa Ofisi ya Itikadi na Siasa ya Amiri Jeshi Mkuu, aliyasema hayo katika awamu ya kumi ya mafunzo ya uelewa na utambuzi (Basirat), yaliyowahusisha manaibu, wakuu wa mashirika na wakurugenzi wakuu wa taasisi ya kuhifadhi kumbukumbu na kueneza maadili ya Ulinzi Mtakatifu na muqawama. Mkutano huo ulifanyika katika Jumba la Makumbusho la Kitaifa la Mapinduzi ya Kiislamu na Ulinzi Mtakatifu.
Akizungumzia umuhimu wa kueneza utamaduni wa kujitolea na shahada, alisema: “Kufikia daraja la shahada ni tawfiki kubwa ambayo hujaaliwa watu maalumu wanaopata uangalizi wa Mwenyezi Mungu.”
Hujjatul-Islam wal-Muslimin Saeedi, akizungumzia pia njama za Marekani dhidi ya Iran, aliongeza kwamba; Wamarekani walitumia njama na mbinu zao zote dhidi ya Iran kwa miaka mingi, lakini hawakufanikiwa. Kwa sababu hiyo, mwaka uliopita waliamua kuingia wenyewe katika uwanja wa mapambano ili kumaliza kila kitu, lakini hawakuweza kupata mafanikio yoyote katika uwanja wa kijeshi na badala yake wakakabiliwa na anguko kubwa.
Mkuu wa Ofisi ya Itikadi na Siasa ya Amiri Jeshi Mkuu aliendelea kusema: “Ni mara ya kwanza ambapo nchi mbili zenye silaha za nyuklia zinahusika kwa wakati mmoja katika vita dhidi ya Iran. Pia, ni mara ya kwanza Iran ikilenga moja kwa moja kambi za Marekani, kuanzia Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) hadi Jordan.”
Akizungumzia mkusanyiko wa meli za kivita za Marekani zilizopangwa dhidi ya Iran na kushindwa kwake katika vita hivyo, alisema kwamba, takribani shabaha 300 katika kambi 15 za kijeshi za Marekani zilipigwa na vikosi vya kijeshi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Aliongeza kuwa Iran, kupitia udhibiti wake juu ya Mlango-Bahari wa Hormuz, iliweza kuionjesha dola kuu ya kibeberu duniani na washirika wake uchungu wa vikwazo. Alibainisha kwamba athari za kufungwa Mlango-Bahari wa Hormuz zinaonekana leo katika maisha na meza za chakula za wananchi wa kila moja ya nchi zilizochukua hatua dhidi ya Iran.
Hujjatul-Islam wal-Muslimin Saeedi alisema kwamba, hii ni mara ya kwanza Iran kuvunja dhana ya kutoshindwa kwa Marekani na utawala wa Kizayuni. Aliongeza kuwa kwa sasa Milango ya Hormuz na wa Bab al-Mandab, ambazo ni njia mbili muhimu za kimkakati, ziko chini ya udhibiti wa Jukwaa la muqawama.
Mkuu huyo wa Ofisi ya Itikadi na Siasa ya Amiri Jeshi Mkuu, akizungumzia mwamko na kusimama taifa kubwa la Iran, alisisitiza kwamba wananchi wa Iran, kupitia kujitokeza kwao mitaani, wameonesha kuwa watayalinda Mapinduzi yao na nchi yao.
Akifafanua sababu za nguvu na uwezo wa Iran, alisema: “Uwezo wa kurutubisha urani katika viwango vya juu, kuwa na rasilimali nyingi za mafuta na gesi, uwezo mkubwa na wa kushangaza wa kiulinzi, kina cha kimkakati cha Iran, kuwa na Mlango-Bahari wa Hormuz, nguvu ya uongozi na mshikamano wa kitaifa ni mambo yanayoonesha nguvu ya Iran.”
Hujjatul-Islam wal-Muslimin Saeedi, akizungumzia pia uwezo mkubwa wa kijeshi wa Iran, alisema kwamba; nchi hiyo ina uwezo wa kipekee katika makombora na ndege zisizo na rubani, na kwamba ilionesha uwezo hilo wazi katika vita dhidi ya Marekani, jambo lililouacha ulimwengu katika mshangao.
Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Mkuu wa Ofisi ya Itikadi na Siasa ya Amiri Jeshi Mkuu alikumbusha kwamba kuimarika kwa nafasi ya taifa la Iran baada ya Vita vya Ramadhani kumedhihirika wazi, na kwamba kuanzia sasa nchi mbalimbali duniani zitauzingatia kwa uzito mkubwa uwezo wa Iran.
Aliendelea kusema kwamba; baada ya Vita vya Ramadhani, mtazamo kuhusu jeshi la Marekani na jeshi la utawala wa Kizayuni kama majeshi yenye nguvu kubwa umebadilika. Imebainika kuwa majeshi hayo yana udhaifu mwingi.
Hujjatul-Islam wal-Muslimin Saeedi alisema kwamba; leo hii baada ya Vita vya Ramadhani, mitazamo ya wananchi wengi na vijana wa Marekani kuhusu Israel imebadilika, na kwamba mtazamo wa zamani waliokuwa nao kuhusu Israel haupo tena kama ulivyokuwa awali. Aidha, nguvu na hadhi ya Marekani vimeporomoka baada ya vita hivyo, huku mfumo wa zamani wa kiusalama kuhusu eneo la Asia Magharibi ukipitia mabadiliko makubwa.
Mkuu wa Ofisi ya Itikadi na Siasa ya Amiri Jeshi Mkuu alisema kuwa; kutokana na Vita vya Ramadhani, uwezo wa kijeshi wa Iran umewekwa wazi, na leo tunaona kwamba uwezo wake wa vifaa vya kijeshi umefahamika duniani kote. Pia, imebainika kwamba Iran inaweza kutumia uwezo wa vita visivyo vya kawaida (asymmetric warfare) kumshinda adui na kupata ushindi katika vita.
Hujjatul-Islam wal-Muslimin Saeedi, akieleza kwamba Vita vya Ramadhani vina mafunzo na mazingatio mengi, alisisitiza kwamba; jambo linalotia wasiwasi zaidi ni kuanzishwa migawanyiko ya kimawazo kinzani isiyo na msingi wala uhalisia. Alisema kwamba kila mtu anapaswa kuepuka kuchochea migawanyiko ya aina hiyo na badala yake kudumisha mshikamano na umoja wa kitaifa chini ya uongozi.
Maoni yako