Jumatatu 5 Oktoba 2026 - 06:15
Yatufaa Tujiepusheni na Kumlaumu Mtu Aliyetubia Dhambi Zake

Hawza/ Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) katika hadithi, anakataza kumlaumu mtu ambaye ametubu madhambi aliyokuwa ameyafanya.

Shirika la Habari la Hawza, limechapisha hadithi ifuatayo kutoka katika kitabu cha Tanbihul-Khawatir.

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema:

«مَنْ عَيَّرَ أَخَاهُ بِذَنْبٍ قَدْ تَابَ مِنْهُ لَمْ يَمُتْ حَتَّى يَعْمَلَهُ.»

“Mtu yeyote atakayemlaumu ndugu yake kwa dhambi ambayo tayari ametubu kutokana nayo, hatakufa mpaka yeye mwenyewe aifanye dhambi hiyo.”

Tanbihul-Khawatir, Juzuu ya 1, uk. 113.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha