Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza Tehran, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, katika tamko lake, huku likikumbuka na kuheshimu kumbukumbu ya mashahidi mashuhuri wa Muqawama wa Kiislamu nchini Iraq, hususan Shahidi Abu Mahdi al-Muhandis, limewapongeza wananchi wenye heshima na ujasiri wa nchi hiyo, safu moja na yenye nguvu ya Muqawama wa Kiislamu, pamoja na wapiganaji waumini na wanamapinduzi wa ulimwengu wa Kiislamu kwa kufukuzwa kwa wavamizi wa Marekani kutoka Iraq.
Maandishi ya tamko hilo ni kama ifuatavyo:
Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu
“Na bila ya shaka neno letu lilikwisha tangulia kwa waja wetu walio tumwa. Hakika wao ndio watakaosaidiwa.”
Qur'an, 37: 171.
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, huku likiheshimu kumbukumbu ya mashahidi mashuhuri wa Muqawama wa Kiislamu nchini Iraq na katika eneo la Asia Magharibi, hususan Kamanda Mkuu Shahidi Haj Qassem Soleimani na Shahidi Abu Mahdi al-Muhandis, pamoja na wapiganaji wote waumini ambao katika miongo miwili ya mapambano dhidi ya wavamizi wa Marekani walifikia daraja ya kuuwawa shahidi, linawapongeza wananchi wenye heshima na ujasiri wa Iraq, safu moja ya Muqawama wa Kiislamu na wapiganaji wanamapinduzi wa ulimwengu wa Kiislamu kwa ushindi huu wa kihistoria.
Kuifukuza Marekani kutoka Iraq ni matokeo ya msimamo thabiti wa wananchi wenye heshima na ujasiri wa nchi hii katika kudumisha uhuru wao. Wananchi wa Iraq, kupitia kusimama kwao kidhamira katika historia, wamethibitisha kwamba; matakwa ya kitaifa ndiyo silaha yenye nguvu zaidi dhidi ya tamaa za watawala wa kibeberu. Kushinda matakwa ya Muqawama ya Iraq yenye kujinasua dhidi ya utawala wa kibeberu dhidi ya uvamizi wa Marekani ni ukurasa wa dhahabu katika historia ya mapambano ya mataifa ya eneo hili ya kutafuta uhuru.
Kufukuzwa wavamizi wa Marekani, kwa hakika, ni kulazimishwa azma thabiti ya Iraq shujaa dhidi ya utawala wa Marekani wa kigaidi na wenye kuchochea vita, pamoja na watawala wasio na busara wa Ikulu ya White House. Marekani, ambayo daima imekuwa ikizungumza kwa lugha ya nguvu, leo imelazimika kuondoka katika ardhi ambayo iliikalia kwa muda wa miongo miwili.
Marekani imeondoka; si kwa njia ya mazungumzo, wala kwa hisani; bali kwa juhudi za taifa lililosimama imara, kwa damu ya wapiganaji waliotoa maisha yao, na kwa matakwa ya Muqawama ambayo hayakuvunjika kamwe. Sasa Iraq, ikiwa imesimama kwa heshima na ikiwa huru, imesimama juu ya magofu ya uvamizi wa miaka ishirini na inatazama kuchomoza alfajiri ya uhuru.
Bila shaka, tukio hili lenye baraka na la kihistoria ni hatua ya kwanza katika kulipiza kisasi cha mashahidi wa Iraq, hususan Abu Mahdi al-Muhandis, na kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu, ulipizaji wa damu ya wapendwa hawa utakamilishwa kwa kuondolewa kikamilifu Marekani katika eneo hili.
Marekani lazima iondoke katika eneo hili na iachie usimamizi wa usalama kwenye mataifa yenyewe. Uzoefu wa miongo miwili ya uvamizi umeonesha kwamba uwepo wa Marekani haukuleta usalama; bali wenyewe ulikuwa chanzo cha ukosefu wa usalama, ugaidi na ukosefu wa utulivu katika Asia Magharibi. Marekani, baada ya miaka ishirini ya uingiliaji wa kijeshi, ikiwa na takribani watu elfu tano waliouawa kwa mujibu wa madai yake yenyewe, ingawa si takwimu halisi, na baada ya kutumia dola trilioni nne, imefukuzwa katika kilele cha chuki na kinyongo cha wananchi wa Iraq. Takwimu hizi zinaonesha kushindwa kukubwa na kwa kuaibisha kwa Marekani.
Kuondoka vikosi vya Marekani kutoka Iraq ni tukio kubwa la kihistoria lenye maana pana na mafanikio makubwa kwa mhimili wa Muqawama. Hakuna shaka kwamba wananchi wenye heshima na ujasiri wa Iraq, kwa kuendeleza harakati hii tukufu, pia watamaliza uingiliaji wa Marekani katika uchumi na mafuta ya nchi yao, na kwa umoja na matakwa ya kitaifa watajiandalia mustakabali wenye mwangaza. Marekani haijawahi kuwa, wala si, tegemeo linaloweza kuaminika; ukweli na hali halisi ya uwanjani inathibitisha kwamba Marekani ni ya kuondoka, na kwamba ni mataifa yenyewe yanayopaswa kujenga nchi zao.
Kwa yakini tunaweza kusema kwamba kuifukuza Marekani kutoka Iraq ni mwanzo wa kuwaondoa katika eneo lote la Asia Magharibi na katika jiografia ya Umma ya Kiislamu. Ushindi huu mkubwa ni matokeo ya matakwa ya kitaifa ya Iraq, juhudi za makundi ya Muqawama, uungaji mkono wa wananchi na hatua madhubuti za serikali ya nchi hii.
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, mwishoni mwa tamko lake, huku likisisitiza ulazima wa serikali, wananchi na vikosi vya Muqawama vya Iraq shujaa kuwa na busara na tahadhari dhidi ya njama na fitina zinazoweza kubuniwa na Marekani na maadui wa nchi hii kwa ajili ya kuleta tena ukosefu wa usalama na ukosefu wa utulivu katika ardhi hii tukufu; kama watoto wa taifa la Iran, linasisitiza kwa uthabiti kwamba; litaendelea kusimama pamoja na mataifa yanayotetea haki na yanayopambana dhidi ya dhuluma katika eneo hili, kwa ajili ya kuisafisha Asia Magharibi kutokana na mabaki machafu ya wavamizi wa Marekani, na vilevile utawala wa Kizayuni unaoua watoto na wenye ubaguzi wa rangi, na halitaacha kusimama hadi kufikiwa ukombozi kamili wa Quds Tukufu.
ولن يجعل الله للكافرين على المؤمنين سبيلا
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu Iran.
Maoni yako