Ijumaa 2 Oktoba 2026 - 15:00
Mazishi ya Shahidi Sheikh Ali al-Mahouzi, miongoni mwa wanazuoni wa Bahrain, katika kitongoji cha kusini mwa Beirut

Hawza/ Sheikh Ali al-Mahouzi, miongoni mwa wanafunzi wa Bahraini wa Hawza ya Najaf Tukufu, ambaye aliuwawa kishahidi katika mashambulizi ya mabomu ya Bint Jbeil alipokuwa akipambana na Wazayuni, amezikwa katika eneo la kusini mwa Beirut.

Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Hizbullah na wafuasi wa Muqawama, Jumatano, 8 Mehr 1405 (30 Septemba 2026), walifanya sherehe za kuuaga na kuusindikiza mwili wa Shahidi Sheikh Ali Jaafar al-Mahouzi, miongoni mwa wanazuoni wa Bahrain, katika makaburi ya Jannat al-Zahra (sa) katika eneo la kusini mwa Beirut; mwili wake ulizikwa kando ya ndugu zake mashahidi ambao walitangulia kuuwawa kishahidi.

Muungano wa Vijana wa Mapinduzi ya 14 Februari wa Bahrain watoa wito wa kushiriki katika mazishi ya Shahidi al-Mahouzi

Hapo awali, Muungano wa Vijana wa Mapinduzi ya 14 Februari wa Bahrain ulikuwa umewaalika wananchi kushiriki katika mazishi ya mpiganaji shahidi, “Sheikh Ali al-Mahouzi,” na kusema: Sherehe za mazishi hayo zitafanyika Jumatano, saa kumi jioni, katika “Raudhat Jannat al-Zahra (sa)”, lililoko katika eneo la “Kafa’at” katika kitongoji cha kusini mwa Beirut.

Inafaa kutajwa kwamba shahidi huyu aliuwawa akiwa anapambana katika njia ya Wilaya, kusini mwa Lebanon; na alikuwa ametoweka wakati wa mapigano ya mwezi Aprili uliopita.

Mazishi ya Shahidi Sheikh Ali al-Mahouzi, miongoni mwa wanazuoni wa Bahrain, katika kitongoji cha kusini mwa Beirut

Baada ya operesheni ngumu za utafutaji wa uwanjani, kufanya mahojiano na mashahidi walioshuhudia tukio hilo kwa macho yao, na kwa ushirikiano wa wanaharakati waliokuwa uwanjani, timu maalumu ya Muungano wa Vijana wa 14 Februari ilifanikiwa kuthibitisha habari za kuuwawa kwake kkshahidi. Alilengwa na mashambulizi ya mabomu ya kikatili ya Wazayuni alipokuwa akitekeleza jukumu lake la kijihadi dhidi ya wavamizi Wazayuni kusini mwa Lebanon.

Kutokana na ukubwa wa mapigano na ugumu wa usafirishaji wakati huo, taasisi husika za afya ziliuhamisha mwili wake kutoka eneo alikouwawa kkshahidi na kuupeleka katika kijiji kingine kusini mwa Lebanon, ambako alizikwa katika mojawapo ya vijiji vya kusini vya Amil (eneo la kusini mwa Lebanon), kilichokuwa karibu na eneo alikouwawa kishahidi.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha