Ijumaa 28 Agosti 2026 - 23:03
Ayatullah Mahdavi-Pour, Atembelea Ofisi ya Sheikh Mkuu wa Shia Tanzania, Ushirikiano wa Kielimu Wasisitizwa

Hawza/ Ofisi ya Maulana Sheikh Hemed Jalala Mwakindenge, Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Tanzania (TIC), jana ilipokea ugeni wa Ayatullah Mahdayi-Pour kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, katika ziara iliyolenga kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya taasisi za kidini na kielimu za Tanzania na Iran.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Mahdavi-Pour aliwasili akiwa ameambatana na Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania pamoja na Mkurugenzi wa Utamaduni wa Iran. Ugeni huo uliifanya ziara hiyo ikiwa sehemu ya juhudi za kuimarisha mahusiano ya kirafiki na ushirikiano katika nyanja mbalimbali, hususan katika eneo la elimu na mahusiano mema ya kitaasisi.

Ziara hiyo pia imekuwa fursa muhimu ya kuimarisha udugu, maelewano na mahusiano mema kati ya taasisi za kidini na kielimu za Tanzania na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, sambamba na kuangalia namna ya kuendeleza juhudi za pamoja katika sekta ya elimu, malezi na huduma kwa jamii.

Akizungumza wakati wa kupokea ugeni huo, Maulana Sheikh Hemed Jalala Mwakindenge aliupongeza ugeni huo na kueleza umuhimu wa kuendeleza ushirikiano kati ya taasisi hizo, huku akisisitiza kuwa elimu ni msingi muhimu wa maendeleo na ustawi wa jamii.

Sheikh Hemed Jalala amesema: Ushirikiano wa kielimu unapaswa kuendelea kupewa kipaumbele, kwa kuwa una nafasi kubwa katika kujenga kizazi chenye maarifa, maadili na uwezo wa kuchangia maendeleo ya jamii, Tanzania na ulimwengu wa Kiislamu kwa ujumla.

Ziara hiyo imehitimishwa kwa kusisitiza umuhimu wa kuendeleza mawasiliano, udugu na ushirikiano wa taasisi za kidini na kielimu, kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Ayatullah Mahdavi-Pour, Atembelea Ofisi ya Sheikh Mkuu wa Shia Tanzania, Ushirikiano wa Kielimu Wasisitizwa

Ayatullah Mahdavi-Pour, Atembelea Ofisi ya Sheikh Mkuu wa Shia Tanzania, Ushirikiano wa Kielimu Wasisitizwa

Ayatullah Mahdavi-Pour, Atembelea Ofisi ya Sheikh Mkuu wa Shia Tanzania, Ushirikiano wa Kielimu Wasisitizwa

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha