Kwa mujibu wa Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, kikinukuu ON4, Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdoğan, katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari pamoja na Rais wa Lebanon, Joseph Aoun, akirejelea kuendelea mashambulizi ya Israel kusini mwa Lebanon, alisisitiza uungaji mkono wa pande zote wa Ankara kwa serikali na wananchi wa Lebanon.
Erdoğan, huku akimshukuru Rais wa Lebanon kwa kufanya ziara nchini Uturuki, ambayo ni ziara ya kwanza ya rais wa Lebanon nchini humo baada ya miaka 17, alisema: Katika mazungumzo yetu na Joseph Aoun, tulijadili mashambulizi yanayoendelea ya Israel kusini mwa Lebanon, njia za kuendeleza uhusiano wa pande mbili, pamoja na maendeleo ya hivi karibuni katika eneo.
Aliongeza kuwa; Uturuki itaendelea kutoa misaada yake ya kibinadamu na kiufundi kwa Lebanon, na inaunga mkono mchakato wa kuimarisha uhusiano na mazungumzo kati ya Lebanon na Syria. Aidha, iko tayari kutoa msaada wowote utakaohitajika katika mwelekeo huo.
Rais wa Uturuki pia, akisisitiza kuendelea kuviunga mkono vikosi vya jeshi la Lebanon, alisema: "Israel inatenda uhalifu dhidi ya ubinadamu."
Erdoğan, akirejelea mashambulizi ya Israel dhidi ya Lebanon, alisema kuwa hadi sasa watu zaidi ya 4,300 wamepoteza maisha katika mashambulizi hayo, na kwamba Uturuki inafuatilia kwa karibu juhudi za kidiplomasia zinazolenga kukomesha mashambulizi hayo na kumaliza uvamizi.
Mwishoni, huku akiwapa pole wananchi wa Lebanon, Erdoğan alisisitiza kuwa Uturuki tangu siku za mwanzo za mgogoro huu imekuwa miongoni mwa nchi zilizolaani kwa kauli kali zaidi vitendo vya kikatili vya Israel.
Maoni yako