Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, polisi wa Uhispania walimkamata mtu huyo wa miaka 55 baada ya kuandika ujumbe na kaulimbiu za chuki dhidi ya Uislamu kwenye kuta za msikiti uliopo mjini Bilbao. Tukio hilo lilifanyika Jumamosi, na baada ya kutekeleza vitendo hivyo vilivyoelezwa kuwa vya ukiukaji wa maadili na uharibifu wa mali ya kitamaduni, alipelekwa katika kituo cha polisi majira ya saa 3:30 asubuhi.
Kwa mujibu wa mashuhuda, polisi wa eneo la Basque (Ertzaintza) walimtambua mtu huyo karibu na msikiti akiwa bado ameshika makopo ya rangi za kupulizia, huku ushahidi ukionesha kuwa alikuwa akieneza propaganda za chuki dhidi ya Uislamu. Ushahidi huo ulisababisha kukamatwa kwake.
Ripoti hiyo inaeleza kuwa; kutokana na kampeni zinazoungwa mkono na makundi ya Kizayuni, vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu vinaendelea kuongezeka barani Ulaya. Mashirika yasiyo ya kiserikali pamoja na wanaharakati wa haki za binadamu wamezitaka mamlaka kuweka sheria madhubuti za kukabiliana na uhalifu wa aina hiyo.
Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na kampuni moja ya utafiti wa takwimu mwezi Machi mwaka huu, karibu asilimia 50 ya Waislamu hukumbana na ubaguzi kila siku, kiwango ambacho ni mara mbili ya kile kinachopatikana kwa idadi ya watu kwa ujumla.
Takwimu hizo pia zinaonesha matokeo ya utafiti wa Wakala wa Umoja wa Ulaya, ambao, kwa mujibu wa ripoti hiyo, unaashiria kuwepo kwa ushawishi wa nyuma ya pazia unaochochea kuenea kwa ubaguzi huo ndani ya mifumo ya Ulaya.
Miongoni mwa nchi za Ulaya, ripoti hiyo inaeleza kuwa; Waislamu wa Uingereza hukumbwa na vitendo vingi zaidi vya ukatili. Polisi wa Uingereza pia wametangaza kuwa watu wengi waliokamatwa kwa tuhuma za kuandaa mashambulizi ya kigaidi yanayohusishwa na misimamo mikali ya mrengo wa kulia walikuwa na umri wa kati ya miaka 27 hadi 82, na wengi wao ni wanaume.
Chanzo: Morocco World News.
Maoni yako