Ijumaa 17 Julai 2026 - 17:00
Mjapani Asilimu Baada ya Kusoma Qur'ani Tukufu

Hawza/ Bw. Kazuki Suleiman Kanehara, raia wa Japan mwenye umri wa miaka 31, ameukumbatia Uislamu kwa moyo mkunjufu baada ya kusoma Qur'ani Tukufu.

Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, kijana huyo wa Kijapani ambaye ni mmiliki wa mgahawa, alisilimu miaka saba iliyopita. Anasema kuwa kusoma Qur'ani Tukufu kulikuwa na nafasi ya msingi katika uamuzi wake wa mwisho wa kuukubali Uislamu. Baada ya kuanza kujifunza kuhusu dini hiyo kupitia rafiki yake Muislamu, mapenzi yake kwa Uislamu yaliendelea kuongezeka siku baada ya siku.

Kazuki Suleiman Kanehara, mwenye umri wa miaka 31 na mkazi wa mji wa Kyoto, alisema kuwa; kwa mara ya kwanza alifauhamu Uislamu akiwa na umri wa miaka 19 alipokuwa akisoma nchini Ujerumani. Huko ndipo alipokutana kwa mara ya kwanza na wanafunzi Waislamu, akazungumza nao na kuwa marafiki zao.

Akizungumza alipokuwa ametembelea mji wa Istanbul akiwa pamoja na rafiki yake Muislamu, Bw. Ismail, alisema: "Mtazamo wangu wa kwanza kuhusu Waislamu ulikuwa kwamba wao ni watu wenye wema mkubwa."

Alieleza kuwa; kabla ya hapo, uelewa wake kuhusu Uislamu ulitokana zaidi na televisheni na filamu za Kijapani, ambazo zilikuwa zikiuonesha Uislamu kwa sura hasi.

Aliongeza: "Rafiki yangu Ismail ndiye aliyenifanya nianze kufanya utafiti na kujifunza kuhusu Uislamu. Alikuwa na subira kubwa na alinifundisha Uislamu, kwa kweli alikuwa mfano mzuri kwangu, siku zote alikuwa mwenye kunifanyia wema, hata nilipokuwa nikikosea, alikuwa kama kaka yangu mkubwa."

Chanzo: AA Agency.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha