Jumatano 15 Julai 2026 - 07:35
Waislamu Wote Walipize Kisasi cha Damu ya Imam Shahidi

Hawza/ Mjumbe wa Mafaqihi wa Baraza la Walinzi wa Katiba amesema: Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: «Hakika sisi ni wenye kulipa kisasi kwa waovu». Hya ni matakwa ya haki. Inshaallah, Waislamu, Mashia na wapenzi wa Ahlul-Bayt (as), kwa kutimia masharti yanayohitajika na kwa kuzingatia pande zote za suala hili, watawalipiza kisasi madhalimu hawa na wauaji wa kiongozi huyo mtukufu pamoja na mashahidi wengine wa jihadi.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Muhammad Mahdi Shab Zendehdar, pembeni mwa hafla ya kumbukumbu ya Imam Shahidi iliyofanyika katika ukumbi wa Shabistan Imam Khomeini (ra) ndani ya Haram Tukufu ya Hadhrat Ma'sumah (as), katika mahojiano na mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, alieleza mambo muhimu kuhusu majukumu ya hawza pamoja na suala la kulipiza kisasi dhidi ya wahusika wa kuuawa kishahidi Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Katibu wa Baraza Kuu la hawza, mwanzoni alizungumzia nafasi ya juu ya Kiongozi Shahidi na kauli zake zenye thamani, akisema: "Katika tamko lake kuhusu 'Hawza iliyo mstari wa mbele na yenye kuongoza', alitoa mawazo ya hali ya juu na ya kipekee. Inshaallah, vyuo vya elimu ya dini viweke tamko hilo mbele ya macho yao na vijitahidi kulitekeleza kwa vitendo."

Mjumbe wa Mafaqihi wa Baraza la Walinzi wa Katiba, akisisitiza kuwa; maelekezo na matakwa ya Kiongozi Shahidi yanapaswa kuwa mhimili wa utekelezaji, alisema: "Inshaallah, yale yote aliyokusudia yatafikiwa. Hawza inapaswa kwa juhudi zote kuendeleza njia iliyochorwa na Imam Shahidi na kutekeleza wajibu wake katika kufanikisha malengo ya Mapinduzi ya Kiislamu."

Ayatullah Shab Zendehdar aliendelea kwa kurejelea ahadi ya Mwenyezi Mungu kuhusu kulipiza kisasi kwa madhalimu, akasema: Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: «إِنَّا مِنَ الْمُجْرِمِینَ مُنْتَقِمُونَ». Haya ni matakwa ya haki. Inshaallah, Waislamu, Mashia na wapenzi wa Ahlul-Bayt (as), kwa kutimia masharti yanayohitajika na kwa kuzingatia pande zote za suala hili, watawalipiza kisasi kwa madhalimu hawa na wauaji wa kiongozi huyo mtukufu pamoja na mashahidi wengine wa jihadi.

Katibu wa Baraza Kuu la hawza, mwishoni mwa mazungumzo yake, alimuomba Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwa Hadhrat Baqiyyatullah al-A'dham (aj), aipe ushindi safu ya haki, na akaeleza matumaini kwamba kwa mshikamano na umoja wa neno, mazingira ya kutimia kwa ahadi hii ya Mwenyezi Mungu yataandaliwa, na damu ya mashahidi itakuwa sababu ya kuharakisha kudhihiri na kuangamia kwa madhalimu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha