Jumamosi 11 Julai 2026 - 13:39
Nukta 12 na Mafunzo ya Kistaarabu ya Tukio la Kihistoria la Mazishi ya Imam Shahidi/ Kulipiza Kisasi kwa Damu ya Bwana Shahidi ni Haki ya Kisheria na ya Kikanuni ya Umma

Hawza/ Khatibu wa Swala ya Ijumaa wa Qum, akifafanua nukta na mafunzo yaliyotokana na ushiriki wa mamilioni ya watu katika mazishi ya kishujaa ya Imam Shahidi, alisisitiza kuwa: Umati wa mamilioni ya washiriki katika mazishi hayo umetuma ujumbe kwa Trump mhalifu na Netanyahu mwovu kwamba; kulipiza kisasi kwa damu ya mashahidi wetu ni jambo la hakika, na wanapaswa kusubiri kisasi hicho.

Kwa mujibu wa mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Alireza A'rafi, katika khutuba za Swala ya Ijumaa ya tarehe 19 Tir 1405 Hijria Shamsia (July 10 2026), iliyofanyika katika Msikiti wa Swala wa Quds mjini Qum, aliwapongeza na kuwashukuru kwa dhati wananchi wa Iran na Iraq kwa tukio lao la kishujaa la mamilioni ya watu katika hafla za kuaga na mazishi ya Imam Shahidi.

Alisema: Imam Shahidi alikuwa ni mfumo kamili wa fikra na shule angavu iliyochipuka kutoka katika Uislamu na fikra za Imam Marehemu, jambo ambalo linahitaji kuchambuliwa kwa kina.

Jumbe na Mafunzo ya Tukio la Kishujaa la Wananchi katika Mazishi ya Bwana Shahidi

Funzo la Kwanza: Kufufuliwa kwa Kaulimbiu ya «إحدی‌الحسنیین» Moja ya vizuri viwili

Imamu wa Ijumaa wa Qum alisema kuwa; mazishi ya kihistoria ya Imam Shahidi wa Umma yalikuwa ni mnyororo wa ustaarabu ulioundwa na Umma wa Kiislamu nchini Iran na Iraq.

Aliendelea kusema: Kwa mara nyingine tena, Mapinduzi ya Kiislamu na taifa la Iran vimeifufua kaulimbiu ya «Moja ya vizuri viwili», vimeinua ari ya kupokea mauti na shahada kwa moyo wa ridhaa, na vimethibitisha ushindi wa damu dhidi ya upanga. Mantiki ya Uislamu na tukio hili la kishujaa mlilolitekeleza ni ushindi wa damu dhidi ya upanga, ushindi wa uthabiti na mapambano dhidi ya ujinga na uovu, pamoja na kupokea shahada kwa moyo wa kujitolea.

Ayatullah A'rafi alisisitiza kuwa; dunia inapaswa kujua kwamba taifa letu linaikaribisha mauti katika njia ya Mwenyezi Mungu, haki na ubinadamu, na kwamba vijana wetu wako tayari kwa jihadi na shahada kwa ajili ya kulinda heshima na utukufu wao, Uislamu na Iran.

Funzo la Pili: "Sisi Tunaweza"

Khatibu wa Swala ya Ijumaa wa Qum aliendelea kusema: Mantiki ya Maimamu wawili wa Mapinduzi ni "Sisi Tunaweza." Imam Marehemu aliiasisi kaulimbiu hiyo, na Kiongozi Shahidi akaidhihirisha kwa vitendo.

Aliyaambia mataifa ya dunia: Ninyi pia mnaweza kutoka katika udhalili, kuonja ladha ya uhuru na kujitegemea, na kutekeleza mambo makubwa; kwa sababu taifa moja limesimama imara mbele ya mashambulizi makubwa ya dola yenye nguvu zaidi kiuchumi na kijeshi duniani.

Mjumbe wa Baraza la Walinzi wa Katiba alisema kuwa; kuundwa kwa mahusiano na mizani mpya duniani kumetokana na uwepo wa wananchi katika medani za mapambano. Akasisitiza kwamba Umma wa Kiislamu unapaswa kuwa macho na kujifunza funzo hili kubwa.

Funzo la Tatu: Nafasi Isiyoweza Kufidiwa ya Irada na Uamsho wa Taifa

Mkurugenzi wa Hawza za nchini Iran, aliendelea kusema kuwa nafasi ya irada na mwamko wa wananchi, pamoja na kuielimisha jamii na kufanya jihadi ya kubainisha ukweli (Jihad Tabyin), ni miongoni mwa mafunzo mengine makubwa yaliyotokana na tukio hili la kishujaa la wananchi.

Funzo la Nne: Nafasi ya Utamaduni na Maadili ya Kidini

Alisema kuwa; nafasi ya utamaduni wa kidini na Ashura, kushikamana na maadili ya Mwenyezi Mungu, Marjaiya ya Kidini na Wilayah ya Mwenyezi Mungu ni misingi muhimu iliyozalisha muujiza huu wa karne na kumfikisha Imam Shahidi kwenye kilele cha utukufu. Alisisitiza kuwa mtaji huu wa imani unapaswa kulindwa kwa nguvu zote.

Imamu wa Ijumaa wa Qum aliongeza kuwa; miongoni mwa maadili hayo, nafasi ya uongozi wa kidini kupitia Wilayat al-Faqih ni nafasi ya juu sana inayopaswa kuhifadhiwa na kuthaminiwa. Alisema kuwa leo pia, katika mwendelezo wa njia yenye nuru ya Maimamu wawili wa Mapinduzi, uongozi wa Ayatullah Sayyid Mujtaba Khamenei umejidhihirisha, na mfumo huu wa maadili unapaswa kulindwa na kuhifadhiwa.

Funzo la Tano: Umuhimu wa Silaha za Kisasa

Alisema kuwa; silaha za kisasa ni mtaji mkuu wa taifa hili ambao haupaswi kupotezwa. Alieleza kuwa tunahitaji nguvu za kiutamaduni, kisiasa, kijamii, kiusalama, kidiplomasia na kiuchumi, lakini tusidanganyike; kwa sababu nguvu za kijeshi na silaha ndio nguzo inayoyawezesha mafanikio ya nyanja zote nyingine.

Mkurugenzi wa Hawza alisisitiza kuwa; taifa letu linasimama imara nyuma ya mfumo wa Kiislamu na vikosi vya ulinzi, na litaendelea kuimarisha uwezo wake wa kijeshi sambamba na sekta nyingine siku baada ya siku.

Funzo la Sita: Heshima na Utukufu wa Taifa la Iran

Khatibu wa Swala ya Ijumaa wa Qum alisema kuwa; maadui walikuwa wamepanga kulilazimisha taifa la Iran kujisalimisha, kulidhalilisha na kuliteketeza, lakini ushiriki wenu umeonesha kwamba hayo yalikuwa ni ndoto za mchana za watu waliopotoka na mipango ya akili zilizochafuliwa na ulevi.

Mkurugenzi wa Hawza alisisitiza kuwa; taifa la Iran, kwa fadhila za Mwenyezi Mungu na licha ya kustahimili kila aina ya ugumu, limetetea heshima, utukufu na adhama yake. Leo maadui wanashuhudia utukufu huo badala ya udhalili walioutamani. Aliongeza: Yapofuke macho yasiyoweza kuuona utukufu, adhama na ustahimilivu wa Iran na Mhimili wa Muqawama. Macho ya Trump pia yalikuwa hayaoni, na mustakabali wenye giza unamsubiri.

Funzo la Saba: Kuendelea kwa Uhai wa Muqawama na Kuchipuka kwa Vizazi Vipya

Ayatullah A'rafi alisema kuwa; kuchipuka kwa vizazi vipya na kukua kwa utamaduni wa Muqawama ni matokeo ya irada ya taifa la Iran na Umma wa Kiislamu. Aliongeza kuwa, kinyume na matarajio yote ya maadui, Mhimili wa Muqawama bado uko hai katika maeneo yake yote ya awali, na hata machipukizi mapya yamejitokeza katika eneo hili. Alisisitiza kuwa, kwa fadhila za Mwenyezi Mungu, kutaundwa mnyororo wenye nguvu zaidi kuliko ule wa miaka miwili iliyopita, ambao utasimama dhidi ya jeshi la Marekani lenye kiu ya damu na utawala haram wa Israel.

Funzo la Nane: Roho na Utambulisho Mmoja wa Ulimwengu wa Kiislamu

Mkurugenzi wa Hawza za Elimu za Kidini nchini Iran, alisema kuwa; mazishi ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi yalidhihirisha kwamba Umma wa Kiislamu una utambulisho mmoja. Alisema kuwa hafla hiyo ilionesha muungano wa nyoyo na nafsi unaovuka mipaka na jiografia. Aliongeza kuwa hili ni miongoni mwa mafanikio ya Imam Shahidi na taifa la Iran, kwani waliweza kuuunganisha Umma wa Kiislamu chini ya bendera moja. Alisisitiza kwamba, kwa msaada wa Mwenyezi Mungu, njia hii itaendelea mbele ya Trump, Netanyahu na maadui wa Uislamu.

Funzo la Tisa: Haki ya Kisheria na Kikanuni ya Kulipiza Kisasi kwa Damu ya Imam Shahidi

Imamu wa Ijumaa wa Qum pia alizungumzia haki ya kisheria na kikanuni ya kulipiza kisasi kwa damu ya Imam Shahidi, kwakusema: Ujumbe uliobebwa na bendera nyekundu za Ashura katika mazishi hayo ulikuwa ni kwamba; kulipiza kisasi kwa damu ya mashahidi na Kiongozi Shahidi ni haki yetu ya kisheria na kikanuni. Alisisitiza kuwa kisasi hicho bado kinasubiri kutekelezwa, na bila shaka kitalipizwa.

Funzo la Kumi: Ujumbe wa Mwamko wa Taifa la Iran kwa Serikali za Kanda

Akizihutubia serikali za eneo hili, alisema: Ujumbe wa mwamko wetu kwa serikali za kanda ni kwamba zijitoe katika utumwa na utegemezi wa mashetani. Msiogope nguvu za Marekani na Israel, bali jitengeni nazo. Yale mnayotuambia kwa siri, yatangazeni hadharani mataifa yenu yatawakubali, lakini endapo mtaendelea na utegemezi huo mtashindwa mbele ya irada ya Mapinduzi ya Kiislamu.

Funzo la Kumi na Moja: Kudhoofika kwa Marekani na Utawala wa Kizayuni

Khatibu wa Swala ya Ijumaa wa Qum aliendelea kusema: Marekani na utawala haram wa Kizayuni wanapaswa kujua kwamba; nguvu zao ziko katika hali ya kudhoofika, na ni lazima waondoke katika eneo hili. Alisema kuwa nguvu ya Uislamu na Muqawama itawafukuza kutoka katika eneo hili na kubadilisha mizani na hesabu za kisiasa zilizopo.

Funzo la Kumi na Mbili: Mfano Mpya wa Ujenzi wa Taifa

Ayatullah A'rafi aliongeza kuwa; mfano wa ujenzi wa taifa unapaswa kujengwa juu ya msingi wa busara ya kimapinduzi na ustahimilivu wa jamii. Alisema kuwa; mihimili ya utendaji, utungaji wa sheria na mahakama, pamoja na taasisi zote za nchi, vinapaswa kubuni dira mpya inayotokana na vita ya tatu, mwangaza wa Mapinduzi ya Kiislamu na urithi mkubwa wa Maimamu wawili wa Mapinduzi.

Mkurugenzi wa Hawza nchini Iran, aliendelea kusema kuwa; kuweka mipango mipya, kujiamini na kutegemea uwezo wa ndani, kutokuwategemea wageni, pamoja na kushikamana na busara ya kimapinduzi na mantiki ya Kiislamu na kimapinduzi, ni miongoni mwa misingi muhimu inayopaswa kuzingatiwa.

Imamu wa Ijumaa wa Qum aliwahutubia viongozi wa nchi kwakusema: Barabara na medani za mapambano ziko pamoja nanyi. Taifa letu kubwa limeikubali mantiki ya Mapinduzi ya Kiislamu, na njia hii inapaswa kujidhihirisha katika maamuzi na mipango yetu yote.

Kuundwa kwa Mnyororo wa Matukio Makubwa ya Kishujaa

Akirejelea kwamba katika wiki iliyopita kulishuhudiwa mnyororo wa matukio makubwa ya kishujaa yaliyokamilisha mapambano ya uwanjani na miezi minne ya vita dhidi ya dola yenye nguvu zaidi duniani, alisema: Mlolongo huu wa wiki moja ulioanzia Karbala, Najaf, Tehran, Qum na Mashhad, na ambao utaendelea katika ulimwengu mzima wa Kiislamu kupitia hafla mbalimbali, ni mnyororo wenye nuru, harakati kubwa ya kistaarabu na tukio la kipekee la kihistoria lililotekelezwa na Umma wa Kiislamu.

Khatibu wa Swala ya Ijumaa wa Qum, akisisitiza kuwa; tukio la mazishi ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ni tukio kubwa la kisiasa na kiimani ambalo limeleta mabadiliko makubwa katika kina cha historia, alisema: Hongera kwa Umma huu unaotambua nyakati, unaofahamu nafasi yake na ambao haukusalimu amri mbele ya dhuluma na umwagaji damu.

Pia aliwashukuru wananchi kwa kuwa na uoni wa mbali na kujitokeza kwa wakati katika nyakati nyeti, na akatoa shukrani kwa viongozi, taasisi zilizotoa msaada na ushirikiano, wahudumu wa mawakibu, Ataba Tukufu na wote walioshiriki na kutoa mchango wao katika kufanikisha shughuli hizo.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha