Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, ufafanuzi wa Ofisi ya Ayatullah al-Udhma Nouri Hamadani kuhusu habari zilizosambazwa kuhusiana na kutokuwepo kwa mtukufu huyo katika hafla ya kuuaga na kuongoza ibada juu ya mwili mtukufu wa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah al-Udhma Imam Khamenei (ra), ni kama ifuatavyo:
Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.
Tunatoa shukrani na pongezi kwa mahudhurio makubwa, yenye hamasa, heshima na yaliyoambatana na uoni wa mbali wa taifa la Iran, lenye dini na uaminifu, pamoja na taifa pendwa la Iraq, katika hafla ya kuuaga mwili mtukufu wa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah al-Udhma Imam Khamenei (ra).
Kutokana na kurudiwa mara kwa mara habari zilizotangazwa na shirika la Redio na Televisheni la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pamoja na baadhi ya vyombo vingine vya habari, kwamba Swala ya Maiti juu ya mwili mtukufu wa Kiongozi Shahidi ingeongozwa na Marjii Mkuu wa Taqlid, Ayatullah al-Udhma Nouri Hamadani (Mola amuhifadhi), katika mji mtukufu wa Mashhad, tunapenda kuwafahamisha yafuatayo:
Pamoja na kwamba maandalizi ya ushiriki wa mtukufu huyo katika hafla hiyo yalikuwa yamefanyiwa tathmini na kuzingatiwa, kutokana na hali ya afya yake, umbali wa safari na kutokuwepo kwa mazingira yanayohitajika kwa ajili ya safari hiyo, haikuwezekana kwake kuhudhuria hafla hiyo.
Aidha, siku kadhaa kabla ya kufanyika kwa hafla hiyo, ilikwishatangazwa kwamba haingewezekana kwa mtukufu huyo kuhudhuria.
Hata hivyo, kwa masikitiko makubwa, licha ya taarifa hiyo kutolewa mapema, baadhi ya vyombo vya habari viliendelea kuripoti hadi saa za mwisho za hafla kwamba mtukufu huyo angehudhuria, jambo lililosababisha kuzuka kwa baadhi ya sintofahamu na mkanganyiko.
Tunatumaini kwamba kwa umakini na juhudi zaidi kutoka kwa wanahabari na vyombo vya habari, kutazuiliwa kutokea kwa sintofahamu zozote pamoja na kusambazwa kwa habari zisizo sahihi.
Maoni yako