Ijumaa 10 Julai 2026 - 12:42
Nairobi Yaungana na Iran Kumuenzi Kiongozi Shahidi; Mamia Wajitokeza Katika Hafla ya Kumbukumbu

Hawza/ Mamia ya waombolezaji nchini Kenya walikusanyika siku ya Jumatano tarehe 8 katika Kituo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran jijini Nairobi, kushiriki hafla maalumu ya kumuenzi Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei. Hafla hiyo ilifanyika kama ishara ya mshikamano na mamilioni ya Wairani waliokuwa wakishiriki katika maandamano makubwa ya mazishi yaliyofanyika kote nchini Iran.

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Hafla hiyo, iliyoandaliwa na Kituo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Kenya, ilihudhuriwa na mamia ya waumini, wanazuoni wa Kiislamu, masheikh, viongozi wa kijamii na kisiasa pamoja na wapenzi wa Ahlul-Bayt (as), waliokusanyika kutoa heshima zao za mwisho kwa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kuonesha mshikamano wao na wananchi wa Iran katika kipindi hiki cha maombolezo.

Washiriki wa hafla hiyo walieleza kuwa; maisha ya Ayatullah Sayyid Ali Khamenei yalikuwa mfano wa uongozi uliojengwa juu ya misingi ya imani, uadilifu, kujitolea na kusimama kidete katika kutetea haki za Waislamu na wanyonge duniani. Aidha, walisisitiza kuwa mchango wake utaendelea kuwa kukumbukwa katika vizazi vijavyo.

Miongoni mwa waliohudhuria hafla hiyo alikuwa ni Sheikh Ali Saamoja, kiongozi wa dini na mwanaharakati mashuhuri nchini Kenya. Katika hotuba yake, alizungumzia wasifu wa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, akielezea nafasi yake katika kuimarisha umoja wa Umma wa Kiislamu, kuendeleza fikra za Muqawama na kusimamia maadili ya Kiislamu kwa ujasiri na busara.

Mwishoni mwa hafla hiyo, Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Kenya pamoja na Mkuu wa Kituo cha Utamaduni cha Iran waliwashukuru kwa dhati waumini na wageni wote waliojitokeza kushiriki katika hafla hiyo. Walieleza kuwa; mahudhurio hayo makubwa yameonesha uhusiano wa kindugu uliopo kati ya wananchi wa Kenya na Iran, pamoja na kuthibitisha kwamba kumbukumbu na misingi aliyoisimamia Kiongozi Shahidi itaendelea kuishi katika nyoyo za watu huru duniani.

Nairobi Yaungana na Iran Kumuenzi Kiongozi Shahidi; Mamia Wajitokeza Katika Hafla ya Kumbukumbu

Nairobi Yaungana na Iran Kumuenzi Kiongozi Shahidi; Mamia Wajitokeza Katika Hafla ya Kumbukumbu

Nairobi Yaungana na Iran Kumuenzi Kiongozi Shahidi; Mamia Wajitokeza Katika Hafla ya Kumbukumbu

Nairobi Yaungana na Iran Kumuenzi Kiongozi Shahidi; Mamia Wajitokeza Katika Hafla ya Kumbukumbu

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha