Ijumaa 10 Julai 2026 - 06:00
Ayatullah A'rafi Apongeza Tukio la Kihistoria la Mazishi ya Mwili Mtukufu wa Imam Shahidi Nchini Iraq

Yaliyotokea nchini Iraq na katika miji ya Najaf na Karbala wakati wa kuusindikiza mwili mtukufu wa Kiongozi Shahidi na Kiongozi wa Umma, Imam Khamenei (ra), yanaonesha kina cha imani, ikhlasi, kujitolea na kujitoa mhanga kwa taifa shupavu la Iraq.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, maelezo kamili ya ujumbe wa Ayatullah A'rafi wa kupongeza tukio la kihistoria la mazishi ya Imam Shahidi katika Iraq yenye heshima na fahari ni kama ifuatavyo:

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

مِّنَ ٱلمُؤمِنِینَ رِجَال صَدَقُواْ مَا عَٰهَدُواْ ٱللَّهَ عَلَیهِ فَمِنهُم مَّن قَضَیٰ نَحبَهُۥ وَمِنهُم مَّن یَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُواْ تَبدِیلا

Amani iwe juu ya Hussein, na juu ya Ali bin Hussein, na juu ya watoto wa Hussein, na juu ya maswahaba wa Hussein.

Yaliyotokea nchini Iraq na katika miji ya Najaf na Karbala wakati wa kuusindikiza mwili mtukufu wa Kiongozi Shahidi na Kiongozi wa Umma, Imam Khamenei (ra), yanaonesha kina cha imani, ikhlasi, kujitolea na kujitoa mhanga kwa taifa shupavu la Iraq.

Utukufu wa uwepo wa wananchi wapendwa wa Iraq, pamoja na makabila yote yenye heshima, makundi mbalimbali ya wanawake, wanaume, vijana wapiganaji, wanazuoni, wasomi wa vyuo vikuu, makundi ya mhimili wa Muqawama kutoka Iraq, Lebanon na nchi nyingine, pamoja na harakati mbalimbali za kijamii na kisiasa, na nafasi ya kuwezesha na kusaidia ya serikali na wananchi wa Iraq, Ataba Takatifu za Najaf na Karbala, hususan Hashd al-Shaabi, vinaonesha uhusiano wa kina wa kihistoria kati ya mataifa mawili na nchi mbili za Iran na Iraq.

Tukio hili kubwa na lisilo na mfano limekuwa ishara ya umoja wa Umma wa Kiislamu unaozunguka mhimili wa malengo ya Mwenyezi Mungu, uhuru kutoka katika nguvu za ubeberu, juhudi za kujinasua kutoka katika utawala wa Marekani, na ukombozi wa ardhi za Kiislamu na Palestina tukufu kutokana na uwepo mchafu wa Marekani na Wazayuni wavamizi.

Hafla hii yenye nuru, chini ya miale ya mwangaza wa mwenye kulala katika haram tukufu na maziko matakatifu ya Amirul-Muuminina Imam Ali bin Abi Talib (as), Imam Hussein bin Ali (as), Abul-Fadhl al-Abbas (as), pamoja na maeneo mengine matakatifu ya Maimamu watakasifu (as) na makaburi ya wanazuoni na mashahidi wakubwa wa Iraq, inatathminiwa kuwa imevuruga hesabu nyingi za maadui wa Umma wa Kiislamu, mataifa mawili ya Iraq na Iran, na mhimili wa Muqawama. Pia imeweka misingi ya hesabu mpya katika mwamko wa Kiislamu, harakati ya kimataifa ya Umma wa Kiislamu, mshikamano wa mataifa kwa ajili ya kuanzisha mfumo mpya wa Kiislamu na huru katika eneo, na kujinasua kutoka ukoloni na ubeberu. Mawimbi yake, kwa msaada wa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kwa baraka za Walii wa Zama (aj), yatakuwa makubwa na ya kudumu.

Kwa ajili ya neema hii kubwa na ufufuo huu mkubwa wa taifa la Iraq, mhimili wa Muqawama na mataifa ya eneo, tunapaswa kuinamisha nyuso zetu mbele ya kizingiti kitakatifu cha Mwenyezi Mungu na kushukuru. Pia nawapongeza na kuwashukuru wananchi wote wa Iraq, serikali na viongozi wake, mhimili wa Muqawama, mataifa ya eneo, na makundi yote pamoja na tabaka zote zilizosimama katika hafla hii, na wale wote waliounga mkono tukio hili kubwa katika siku za maombolezo ya Bwana wa Mashahidi (as) na Imam Sajjad (as).

Ni wajibu kutoa shukrani za pekee kwa uwepo mkubwa na wa kusifiwa wa viongozi na wahudumu wa Ataba Takatifu, wanazuoni wakuu, wanazuoni wa Hawza, Hawza ya kale na ya kihistoria ya Najaf Ashraf, wanafunzi na wasomi wapendwa wa Iran, Iraq na mataifa mengine katika Hawza hiyo tukufu, pamoja na kundi kubwa la viongozi wa Hawza ya Qum, Jumuiya ya Walimu, Baraza Kuu la Hawza na taasisi za juu za Hawza kutoka Qum, na hasa Marjaiyyah Kuu ya Najaf Ashraf.

Natumaini kwamba kwa uongozi wa Marjaiyah tukufu ya Najaf Ashraf na Qum Tukufu, uhusiano wa Hawza mbili za kihistoria na zinazoongoza Umma Najaf na Qum, pamoja na uhusiano wa mataifa ya Kiislamu, mhimili wa Muqawama na mataifa mawili ya Iraq na Iran katika njia ya malengo makuu ya Kiislamu utaimarika zaidi; na harakati kuelekea ustaarabu mpya wa Kiislamu na kuchomoza kwa jua la Wilaya Kuu la Imam Mahdi (aj) itaendelea kwa kasi zaidi. Pia, katika kuendeleza uhusiano wa mataifa mawili na mshikamano wao wa kusifika katika Arubaini ya Imam Hussein (as) na katika kukabiliana na mashambulizi ya maadui, wataandika hatua mpya na muhimu ya kihistoria.

Nina matumaini ya hakika kwamba kwa uongozi wa Walii Faqihi na Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu (ra), na kwa kujitoa mhanga mataifa ya Kiislamu, taifa la Iran na Iraq na mhimili wa Muqawama, tutashuhudia kudhoofika kwa nguvu za kishetani, kuchomoza kwa nguvu za Uislamu na ushindi wa Umma wa Kiislamu nchini Iran, Iraq na duniani kote. Na kwamba Hawza zote za na mataifa ya Kiislamu vitaendelea kuwa thabiti katika ahadi yao kwa Mawalii wa Mwenyezi Mungu, mashahidi wakuu, viongozi wa dini, Marajii wakuu, Imam Khomeini Mkuu (ra), Imam Khamenei Shahidi (ra), na Kiongozi Mkuu (Mola amuhifadhi).

Alireza A'rafi
Mkurugenzi wa Hawza za Elimu ya Dini

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha