Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Jumatano tarehe 17 Tir 1405 Shamsia (July 8 2026), Iraq imeshuhudia mahudhurio makubwa na yasiyo na mfano ya makundi mbalimbali ya wananchi katika mazishi ya kihistoria ya mwili wa Imam Sayyid Ali Khamenei pamoja na familia yake ya kishahidi. Hafla hiyo inafanyika katika miji mitakatifu ya Najaf Ashraf na Karbala Mualla, huku ikihudhuriwa na wananchi kutoka makabila, jamii na mikondo mbalimbali ya Iraq.
Washiriki wa hafla hiyo, kupitia mahudhurio yao ya hamasa na kaulimbiu za kidini na za kishujaa walizokuwa wakizipaza, walionesha huzuni yao kubwa huku wakisisitiza kuendelezwa kwa njia ya Muqawama na kulindwa kwa umoja wa Umma wa Kiislamu. Mazingira ya hafla hiyo yalijaa hisia, machozi, dua na mshikamano, huku wengi wa waliohudhuria wakieleza kuwa ushiriki wao ni uhuishaji wa ahadi kwa malengo ya Uislamu, Marjaiyya na Muqawama wa Kiislamu.
Kwa mujibu wa wachambuzi, mahudhurio makubwa ya wakazi wa Najaf katika hafla hiyo ni ishara ya uhusiano wa kina uliopo kati ya wananchi wa Iraq, Marjaiyya ya Kishia, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Mhimili wa Muqawama; uhusiano uliojengwa juu ya misingi ya imani ya dini, historia ya pamoja na malengo yanayofanana.
Washiriki walisisitiza kuwa mkusanyiko huo mkubwa, mbali na kuonesha umoja na mshikamano wa mataifa ya eneo hili, unabeba ujumbe wa wazi kwamba Mhimili wa Muqawama bado unaungwa mkono na wananchi, na kwamba tishio au shinikizo lolote dhidi yake litakabiliwa na umoja na uimara wa mataifa ya Kiislamu.
Shughuli za mazishi zimeendelea tangu jana usiku baada ya mapokezi yaliyofanywa na viongozi wa Iraq na Iran katika uwanja wa ndege. Baadaye, hafla iliendelea kwa ushiriki wa umati mkubwa wa waombolezaji, usomaji wa Qur'ani Tukufu, nyimbo za maombolezo na kaulimbiu za kuhimiza umoja. Hafla hiyo imeonesha taswira za kudumu za mapenzi, uaminifu na mshikamano wa wananchi wa Iraq kwa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.
Waziri Mkuu wa Iraq, Ali Falih al-Zaidi, aliwasili katika mkoa wa Najaf Ashraf kwa ajili ya kushiriki katika hafla ya kuupokea mwili wa Imam Shahidi Sayyid Ali Khamenei.
Ofisi ya Habari ya Waziri Mkuu ilisema katika taarifa yake kwamba; Waziri Mkuu Ali Falih al-Zaidi amewasili Najaf Ashraf ili kushiriki katika mapokezi ya mwili wa Kiongozi Shahidi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Marjii Mkuu wa Kidini, Ayatullah al-Udhma Sayyid Ali Husseini Khamenei.
Brigedia Saad Maan, msemaji rasmi wa Kamati Kuu ya Mazishi ya Kiongozi Shahidi wa Iran nchini Iraq, alisema katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari akiwa pamoja na Gavana wa Najaf Ashraf, Yusuf Kanawi, kwamba maandalizi yote ya mazishi ya Kiongozi Shahidi, Hadhrat Ayatullah al-Udhma Imam Sayyid Ali Khamenei, ndani ya Karbala Mualla na Najaf Ashraf yamekamilika. Aliongeza kuwa; zaidi ya waandishi wa habari 3,000 watashiriki katika kuripoti hafla hiyo.
Kwa mujibu wa msemaji rasmi wa Kamati Kuu ya Mazishi ya Kiongozi Shahidi wa Iran nchini Iraq, takribani waombolezaji milioni 3.8 walihudhuria mazishi ya Kiongozi Shahidi wa Umma mjini Najaf.
Hakika, wananchi wa Najaf walitoa mfano wa hali ya juu wa ukarimu katika kumpokea Imam Shahidi wa Umma wa Kiislamu, wakidhihirisha mbele ya ulimwengu uaminifu wao kwa njia na malengo ya Kiongozi Shahidi wa Umma. Hatimaye, baada ya Ayatullah Sayyid Muhammad Taqi al-Hakim kuongoza swala ya maiti juu ya mwili mtukufu wa Imam Shahidi, mwili huo ulizungushwa katika Haram Tukufu ya Amirul-Muuminin (as), na wananchi kutoa heshima zao za mwisho, mwili wake ulielekea Karbala Mualla.
************************"
Majira ya saa 11:00 jioni, kusubiri kwa wapenzi wa Karbala kwa shujaa huyo mkubwa wa Iran na Kiongozi wa Umma kulifikia hatam, ambapo mwili mtukufu wa Imam Shahidi wa Umma uliwasili Karbala Mualla.
Kwa mujibu wa taarifa za viongozi wa mji wa Karbala Mualla, zaidi ya watu milioni 4 walishiriki katika mazishi ya mwili mtukufu wa Kiongozi wa Umma.
Kutokana na msongamano mkubwa wa watu, gari lililokuwa limebeba mwili wa Kiongozi wa Umma wa Kiislamu lilikuwa likisonga polepole kuelekea eneo la Bayn al-Haramayn.
Mamilioni ya watu walikuwa wamekusanyika pembezoni mwa Bayn al-Haramayn wakisubiri kwa hamu kuupokea mwili wa kiongozi wao mpendwa.
Waandaaji wa mazishi hayo makubwa mjini Karbala walipanga kusambaza katika mji mzima wa Karbala sauti ya Kiongozi Shahidi wa Umma akitamka kaulimbiu za "Labbaik Ya Hussein" na "Assalamu Alayka Ya Aba Abdillah", ili mamilioni ya waombolezaji waiitikie kwa pamoja.
Kaulimbiu za "Mauti kwa Marekani" na "Mauti kwa Israel" zilisikika kila pembe ya Karbala Mualla kutoka kwa wakazi na mazuwari wa Haram ya Imam Hussein (as) waliokuwa wakishiriki katika mazishi ya Kiongozi wa Umma.
Mahudhurio hayo ya kishujaa ya mamilioni ya watu katika mazishi ya mwili mtukufu wa Imam Shahidi wa Umma ndiyo jibu ambalo Washington na utawala wa Kizayuni, licha ya kutumia zana zao zote, bado wameshindwa kufahamu maana yake. Mahudhurio hayo ya mamilioni ya watu yalikuwa zaidi ya hafla ya mazishi; yalikuwa ni sauti ya kuonesha kuendelea kwa mshikamano wa Umma na uimara wa Mhimili wa Muqawama. Ujumbe wake ulikuwa wazi kwamba mipango yote ya maadui ya kuleta mgawanyiko miongoni mwa mataifa ya eneo hili imegeuka kuwa majivu mbele ya umoja huo.
Lakini kwa hakika, haifai kupuuza mtazamo wa Tauhidi katika mahudhurio haya ya kishujaa ya wananchi. Yule aliyeziunganisha nyoyo za watu kwa Kiongozi Shahidi ni Mwenyezi Mungu; kwa kuwa Kiongozi Shahidi alikuwa miongoni mwa watu wa imani na matendo mema. Ndiyo maana Mola Mtukufu aliweka mapenzi yake ndani ya nyoyo za watu.
﴿إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ سَيَجْعَلُ لَهُمُ الرَّحْمَٰنُ وُدًّا﴾
Bila shaka wale walioamini na wakatenda mema, Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema atawawekea mapenzi ndani ya nyoyo za watu.
(Surat Maryam, Aya ya 96).
Aidha, inaweza kusemwa kwamba; miongoni mwa matendo mema yaliyompamba Kiongozi wa Umma kwa imani ya kweli ni kusimama imara mbele ya kambi ya ukafiri na matwaghuti, kama ambavyo Mwenyezi Mungu Mmoja anavyosema katika Qur'ani Tukufu:
﴿وَلَا يَطَئُونَ مَوْطِئًا يَغِيظُ الْكُفَّارَ وَلَا يَنَالُونَ مِنْ عَدُوٍّ نَّيْلًا إِلَّا كُتِبَ لَهُم بِهِ عَمَلٌ صَالِحٌ ۚ إِنَّ اللَّهَ لَا يُضِيعُ أَجْرَ الْمُحْسِنِينَ﴾
Wala hawapigi hatua yoyote inayowaghadhibisha makafiri, wala hawapati madhara yoyote kutoka kwa adui, isipokuwa huandikiwa kwa sababu hiyo tendo jema. Hakika Mwenyezi Mungu hawapotezi malipo ya watenda mema.
(Surat at-Tawbah, Aya ya 120).
Sifa hii ya kuwaghadhibisha makafiri na maadui wa Mwenyezi Mungu ndiyo sifa ambayo viongozi wengi wa Umma wa Kiislamu leo hawana.
Na sasa, mwili wa mbeba bendera ya mapambano dhidi ya kambi ya matwaghuti uko njiani kuelekea katika Haram ya mbeba bendera wa Karbala.
Ewe Bwana wangu! Ewe Imam wangu Shahidi! Tunakuomba usitusahau utakapowasili katika Haram ya mpendwa wako. Mikono yetu iliyo mitupu imeelekezwa kwenye mikono yako iliyojaa rehema ili ituinue kwa dua mbele ya Mwenyezi Mungu; kwani dua zako kwa ajili yetu ni zenye kukubaliwa. Wewe ni mpendwa wa Mwenyezi Mungu. Sasa umekuwa jirani na mwenza wa Abaa Abdillahi al-Hussein (as).
Kwa takribani saa nne na nusu usiku, mwili mtukufu wa Kiongozi Shahidi ulikuwa ukisindikizwa katika mji wa Karbala, na kutokana na mahudhurio makubwa yenye hamasa ya wananchi wa Iraq, bado haukufika katika eneo la Bayn al-Haramayn.
Majira ya saa 3:15 usiku kwa saa za Iran. Ilikadiriwa kuwa mwili wa Imam Shahidi utawasili Bayn al-Haramayn baada ya takribani saa mbili zijazo.
Uongozi wa Haram Tukufu ya Imam Hussein (as) umetangaza katika taarifa kwamba bendera ya Imam Hussein (as) itawekwa juu ya jeneza la Imam Shahidi.
Najaf na Karbala Zashuhudia Mahudhurio Makubwa ya Wananchi wa Iraq katika Mazishi ya Mbeba Bendera ya Mapambano Dhidi ya Matwaghuti
Najaf na Karbala Zashuhudia Mahudhurio Makubwa ya Wananchi wa Iraq katika Mazishi ya Mbeba Bendera ya Mapambano Dhidi ya Matwaghuti
Najaf na Karbala Zashuhudia Mahudhurio Makubwa ya Wananchi wa Iraq katika Mazishi ya Mbeba Bendera ya Mapambano Dhidi ya Matwaghuti
Najaf na Karbala Zashuhudia Mahudhurio Makubwa ya Wananchi wa Iraq katika Mazishi ya Mbeba Bendera ya Mapambano Dhidi ya Matwaghuti
Najaf na Karbala Zashuhudia Mahudhurio Makubwa ya Wananchi wa Iraq katika Mazishi ya Mbeba Bendera ya Mapambano Dhidi ya Matwaghuti
Najaf na Karbala Zashuhudia Mahudhurio Makubwa ya Wananchi wa Iraq katika Mazishi ya Mbeba Bendera ya Mapambano Dhidi ya Matwaghuti
Picha:




Maoni yako