Jumatatu 15 Juni 2026 - 16:00
Hafla ya Kumuenzi Ayatullah al-Udhma Fayyadh Yafanyika kwa Uratibu Uliopangwa na Haram Takatifu ya Hussein na Abbasi kati ya Haram Mbili Karbala

Hawza/ Hafla ya kumuenzi Ayatullah al-Udhma Muhammad Is’haq Fayyadh imefanyika kwa uratibu wa Haram Takatifu ya Husseini na Haram Takatifu ya Abbasi, kwa kuhudhuriwa na wawakilishi wa Ayatullah al-Udhma Sistani katika eneo la Bainal-Haramayn.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, hafla ya kumuenzi marehemu Ayatullah Sheikh Muhammad Is’haq Fayyadh, mmoja wa Marjaa waliotangulia mbele ya haki wa Najaf Ashraf, ilifanyika ndani ya Bainal-Haramayn  Karbala Tukufu, kwa uratibu wa Haram Takatifu ya Imam Hussein (as) na Haram Takatifu ya Abbasi (sa).

Katika hafla hiyo, alihudhuria Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Ahmad Safi, msimamizi wa kisheria wa Haram ya Hazrat Abul-Fadhl al-Abbas (as), na Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sheikh Abdul-Mahdi Karbalai, msimamizi wa kisheria wa Haram ya Hazrat Aba Abdillah al-Hussein (as), pamoja na mazuwaru wa haram mbili tukufu na kundi la viongozi wa taasisi hizo mbili. Vilevile zilihudhuria shakhsia mbalimbali za kidini, viongozi rasmi, wataalamu wa vyuo vikuu, kundi la Waumini na wanafunzi wa elimu za dini.

Waliohudhuria walitoa pole na rambirambi zao kwa familia na wapenzi wa marehemu huyo, na wakamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu amrehemu kwa rehema Zake pana, amuingize Peponi, na awajalie waliobaki subira na uvumilivu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha