Kwa mujibu wa Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Qadir Akaras, Rais wa Jumuiya ya Wanazuoni wa Ahlul-Bayt (Ehla-Der) yenye makao yake Istanbul na mmoja wa wanaharakati mashuhuri wa jamii ya wanazuoni wa Ahlul-Bayt nchini Uturuki, katika mahojiano na Shirika la Habari la Hawza, alizungumzia matokeo ya vita vya hivi karibuni dhidi ya Iran, kuundwa kwa utamaduni wa Muqawama katika jamii ya Iran, pamoja na athari za fikra za Imam Khomeini (r.a) katika maendeleo ya sasa. Haya hapa ni mahojiano hayo:
Kwanza tunakushukuru kwa kukubali mwaliko wetu wa mahojiano haya. Tangu siku ya kwanza ya vita vilivyoanzishwa kwa mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran, mshikamano na uhamasishaji wa wananchi barabarani na kwenye viwanja vya umma umevutia hisia za wengi. Katika siku hizi 100, ukiwa mtu anayefuatilia matukio kutoka Uturuki, unautathminije mshikamano huu wa kijamii? Na kwa maoni yako, ujumbe wa watu wa Iran kwa dunia ni upi?
Kwanza nami pia nawapongeza kwa juhudi zenu za kuifikisha sauti ya ukweli na kwa kuuliza maswali haya muhimu. Siku hizi 100 ngumu zimeonesha tena jinsi misingi ya Mapinduzi ya Kiislamu ilivyo imara.
Makosa makubwa ya Marekani, utawala wa Kizayuni na madola ya Magharibi ni kuichambua Iran kana kwamba ni dola ya kawaida ya kitaifa, ilhali wanakabiliana na taifa linalopata nguvu zake kutoka katika imani na ambalo halioni shahada kuwa mwisho, bali linaiona kuwa ushindi.
Mshikamano wa kipekee ambao mimi mwenyewe niliushuhudia wakati wa safari yangu nchini Iran unawasilisha ujumbe huu kwa dunia na hasa kwa madhalimu wa kimataifa: "Hamtaweza kutupigisha magoti kwa vikwazo, mabomu au uchochezi wa ndani. Sisi ni watoto wa shule inayotanguliza heshima mbele ya udhalili."
Uhamasishaji huu umeonesha kwamba mhimili wa Muqawama si muundo wa kijeshi pekee, bali ni mfumo mpana wa kifikra na kijamii unaofanya kazi bila kujali kabila, madhehebu au tofauti nyinginezo.
Tofauti kati ya taswira ya vyombo vya habari na hali halisi nchini Iran
Katika kipindi hiki uliweza pia kusafiri kwenda Iran, kulikuwa na tofauti gani kati ya picha inayotolewa na vyombo vya habari vya kimataifa na hali halisi uliyoiona?
Vyombo vya habari vya Kizayuni na vya Magharibi kwa miaka mingi vimejaribu kueneza picha ys kwamba Iran imegawanyika na iko katika hali ya kusambaratika, na kwamba mfumo wake unategemea mtu mmoja tu kiasi kwamba kuondolewa kwake kungeusambaratisha.
Lakini nilichokiona uwanjani kilikuwa kinyume kabisa na taswira hiyo, katika miji mbalimbali niliona utulivu wa kina, tawakkul na imani thabiti ya wananchi kwa mfumo wao, taswira inayotolewa na vyombo vya habari ya jamii yenye misukosuko iliyogawanyika na iliyo karibu kusambaratika ni ya uongo kabisa. Kinyume chake, tishio la nje limeyafanya makabila na makundi yote kukusanyika katika umoja wa kweli.
Kuhusu mradi wa kijamii unaohusiana na watoto na walimu waliouawa Minab
Katika siku ya kwanza ya vita na kufuatia mashambulizi ya Marekani, watoto na walimu 168 waliuawa kishahidi katika shule moja mjini Minab, tafadhali eleza kuhusu mradi wa kijamii unaohusiana na tukio hili.
Kuuawa kishahidi kwa watoto na walimu 168 katika mazingira ya elimu ni mojawapo ya mifano iliyo wazi zaidi ya uhalifu usio na mipaka wa Uzayuni na ubeberu wa Marekani.
Sisi nchini Uturuki, kama marafiki wa mhimili wa Muqawama, hatukuweza kubaki bila kujali maumivu haya.
Kwa ajili ya kuhifadhi kumbukumbu za mashahidi hawa, chini ya uongozi wa EHLADER na taasisi za Kauthar, pamoja na ushirikiano wa Jumuiya ya Kimataifa ya Misaada ya Kibinadamu ya Kauthar, tulianzisha mradi mkubwa wa mshikamano na ujenzi upya. Mradi huu unajumuisha kujenga upya miundombinu ya elimu katika eneo hilo pamoja na kuandaa programu za kuwaenzi mashahidi.
Pia, wakati wa safari yetu nchini Iran tulifikia makubaliano na Wizara ya Elimu, na kupitia itifaki rasmi tukachukua jukumu la kujenga moja ya shule za Minab. Inshaallah, kabla ya kuanza mwaka mpya wa masomo, “Shule ya Urafiki wa Iran na Uturuki” mjini Minab itajengwa na kuanza kufanya kazi. Lengo letu ni kufufua matumaini yaliyoharibiwa na dhulma, kwa sababu damu iliyomwagika pale ni damu ya watoto wetu.
Maoni yako