Alhamisi 11 Juni 2026 - 09:17
Mikakati 6 Muhimu ya Utoaji Huduma kwa Wanaharakati wa Hawza/ Hawza ni Mtumishi wa Watu Wapendwa

Hawza/ Mkuu wa Hawza nchini Iran alisisitiza kuwa: Bila shaka, Hawza katika historia yake daima hazikuwa taasisi za elimu na ufundishaji pekee, bali sambamba na kubainisha maarifa ya Mwenyezi Mungu, zimekuwa na uwepo hai, wa kutia hamasa na wa kutoa suluhisho katika nyanja za kijamii, kitamaduni, kimaadili na za wananchi.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, matini kamili ya ujumbe wa Ayatullah Alireza A'rafi, Mkuu wa Hawza nchini Iran, kwenye kongamano la “Hawza ya Kielimu Bora na Inayoongoza; Kutoka Ujumbe wa Kimkakati hadi Harakati za Kijamii za Wananchi” ni kama ifuatavyo:

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

Salaam na rehma za Mwenyezi Mungu Mtukufu ziwashukie mashahidi wote wa Mapinduzi ya Kiislamu, hususan Bwana wa Mashahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Imam Khamenei (Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake), familia tukufu za mashahidi, taifa kubwa la Iran, na ninyi wasomi, watu wa thamani wa Hawza za Kielimu, wanaharakati wa kijamii wenye imani na wanaojali, pamoja na watu wa fikra na vitendo katika nyanja za wananchi.

Ninatoa pongezi kwa waandalizi wote, wahusika na washiriki wa kongamano lenye thamani la “Hawza ya Kielimu Bora na Inayoongoza; Kutoka Ujumbe wa Kimkakati hadi Harakati za Kijamii za Wananchi.” Mkutano huu ni ishara wazi ya uchangamfu, uwajibikaji na uwepo wenye athari wa Hawza za Kielimu katikati ya mahitaji ya jamii na katika medani ya kuwahudumia wananchi wapendwa wa Iran ya Kiislamu.

Bila shaka, Hawza katika historia yake daima hazikuwa taasisi za elimu na ufundishaji pekee, bali sambamba na kubainisha maarifa ya Mwenyezi Mungu, zimekuwa na uwepo hai, wa kutia hamasa na wa kutoa suluhisho katika nyanja za kijamii, kitamaduni, kimaadili na za wananchi.

Leo pia, zaidi ya wakati wowote mwingine, matarajio kutoka Hawza ni kwamba; huku ikihifadhi misingi yake ya kielimu na kiroho, iwe na uwepo wa kuongoza wenye hekima na wenye athari katika medani ya harakati za kijamii, utatuzi wa matatizo halisi ya watu na kujibu mahitaji mapya yanayojitokeza katika jamii.

Ni mafanikio na heshima kubwa kwamba kundi la wanaharakati wa kijamii wa Hawza kutoka kote nchini Iran, pamoja na wasimamizi wa taasisi za kiraia za Hawza, wamekusanyika katika mkusanyiko huu ili kujadiliana na kubadilishana mawazo kuhusu uhusiano kati ya ujumbe wa kimkakati wa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu na harakati za kijamii za wananchi.

Mkusanyiko huu ni fursa adhimu ya kutafakari upya uwezo mkubwa wa Hawza katika nyanja za afya ya kijamii, kuondoa madhara ya kijamii, kuimarisha mtaji wa kijamii na kupanua huduma kwa wananchi.

Katika muktadha huu, ningependa kukumbushia mambo kadhaa ya kimkakati ili kuuelekeza kwa ufanisi zaidi utoaji huduma wa wanaharakati wa Hawza:

1. Tathmini sahihi ya mahitaji na kuzingatia matatizo halisi

Utoaji huduma za kijamii unapaswa kujengwa juu ya utambuzi wa kweli wa mahitaji ya jamii, vipaumbele vya maeneo husika na matatizo halisi ya wananchi; si kwa msingi wa matakwa binafsi, hisia au harakati za muda mfupi tu.

2. Kujengwa juu ya wananchi na kuepuka urasimu usio wa lazima

Harakati za Hawza huwa na athari zaidi pale zinapo washirikisha wananchi, kuamsha uwezo wa wananchi na kujiepusha na kubadilika mifumo mizito na isiyo na mwendo.

3. Kuimarisha ushirikiano, kuunda mitandao na kuzuia kurudia kazi

Moja ya mahitaji muhimu ni kuunganisha wanaharakati wa Hawza, taasisi za kiraia, taasisi za kitamaduni na kijamii pamoja na makundi ya jihadi ya kujitolea, ili uwezo uliopo utumike kwa mfumo mmoja ulioratibiwa na wenye malengo badala ya kutawanyika.

4. Kuunganisha uadilifu wa kiakili, kiroho na ufanisi

Huduma za kijamii za Hawza zinapaswa kuwa na msingi wa kielimu na kimaadili, pamoja na busara na usimamizi wa utekelezaji, na pia ziwe zinazoweza kupimika na kulenga matokeo, ili athari zake katika maisha ya watu ziwe dhahiri na za kudumu.

5. Kutilia mkazo malezi ya viongozi wa kati na kizazi kipya cha wanaharakati wa Hawza

Mwendelezo na maendeleo ya njia hii yanahitaji kulea watu wenye imani, uwezo, ubunifu na uelewa wa masuala ya wakati, ili harakati hii isitegemee watu wachache pekee bali igeuke kuwa mkondo endelevu.

6. Kutoa kipaumbele kwa matatizo halisi na ya dharura kwenye jamii

Masuala kama afya ya kijamii, kuimarisha familia, matatizo ya kimaadili, umaskini, kunyimwa fursa, uraibu wa dawa za kulevya, upweke wa kijamii na migogoro ya utambulisho ni miongoni mwa nyanja ambazo Hawza inaweza kuwa na mchango wenye athari na kuunda nafasi ya uongozi wa kijamii.

Mimi binafsi, licha ya hamu na shauku kubwa, kutokana na mazingira yaliyojitokeza nimekosa fursa ya kuwa pamoja nanyi wapendwa na kushiriki katika kikao hiki chenye thamani kubwa. Kwa moyo wa dhati nilitamani kuwepo katika mkusanyiko wenu wenye nuru na baraka nyingi. Hata hivyo, nikiwa mbali, ninaona kufanyika kwa kongamano hili kuwa chanzo cha matumaini, uchangamfu na kuimarika kwa uhusiano kati ya Hawza na jamii, na ninamuomba Mwenyezi Mungu awajalie nyote mafanikio, athari njema na maendeleo ya kila siku.

Inatarajiwa kwamba mkutano huu uwe mwanzo wa hatua zilizo na elimu zaidi, mshikamano zaidi na ukaribu zaidi kwa wananchi katika njia ya kuziendeleza Hawza za Kielimu na kutoa huduma za dhati kwa makundi yote ya jamii, na kwamba matunda yake yaonekane wazi katika kuinua afya ya kiroho, kijamii na kitamaduni nchini.

Ninamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu awajalie nyote mafanikio, afya njema na heshima.

Wassalamu Alaikum wa Rahmatullahi wa Barakatuh

Alireza A'rafi
Mkuu wa Hawza za Kielimu Iran.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha