Alhamisi 4 Juni 2026 - 23:31
Utaratibu wa ratiba ya mazishi na kuzikwa mwili wa Ayatullah al-Udhma Fayyadh watangazwa

Hawza/ Maelezo ya ratiba ya mazishi ya mwili wa Ayatullah al-Udhma Sheikh Muhammad Is’haq Fayyadh, ambaye leo Alhamisi ameaga dunia, yametangazwa.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, maelezo ya ratiba ya kuzikwa mwili wa Marji' mkubwa wa kidini, Ayatullah al-Udhma Sheikh Muhammad Is’haq Fayyadh, ambaye leo Alhamisi ameaga dunia, yametangazwa.

Kwa mujibu wa chanzo kimoja chenye taarifa sahihi, mwili wa marehemu Ayatullah Fayyadh kesho Ijumaa saa tatu asubuhi utasindikizwa kutoka Husseinia ya Aal Yasin iliyopo Kadhimayn Tukufu kuelekea katika Haram Tukufu ya Maimamu wawili wa Kadhimayn (as).

Chanzo hicho kiliongeza kuwa, kisha mwili wake mtukufu kesho Ijumaa saa kumi na moja jioni huko Karbala Tukufu utasindikizwa kutoka Haram ya Hadhrat Abul-Fadhl Abbas (as) kuelekea katika Haram Tukufu ya Imam Hussein (as).

Aidha, chanzo hicho kilisisitiza kwamba; hafla ya kusindikiza mwili wake huko Najaf Ashraf itafanyika Jumamosi ijayo saa tatu asubuhi, kuanzia katika ofisi ya Marji' huyo marehemu kuelekea katika Haram Tukufu ya Imam Ali (as).

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha