Jumanne 26 Mei 2026 - 10:00
Rekodi ya Wiki 129 za Mfululizo ya Kuiunga Mkono Ghaza yawekwa nchini Tunisia

Hawza/ Kwa kaulimbiu ya “Pamoja kwa ajili ya kuvunja mzingiro”, mapigo ya moyo ya mitaa ya Tunisia yanaendelea kwa uthabiti na bila kuyumba, yakisisitiza kwamba; dira ya Palestina katika nyoyo za Watunisia si kaulimbiu tu.

Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, kwa kaulimbiu isemayo “Pamoja kwa ajili ya kuvunja mzingiro”, mapigo ya moyo ya mitaa ya Tunisia yanaendelea kwa uthabiti na bila kuyumba, yakisisitiza kwamba; dira ya Palestina katika nyoyo za Watunisia si kaulimbiu tu, bali ni utambulisho unaojidhihirisha kila wiki mbele ya Ukumbi wa Manispaa katikati ya mji mkuu wa Tunisia. Hali hii imeongezeka pamoja na mfululizo wa harakati za kuunga mkono suala la Palestina, Ghaza na mhimili wa Muqawama katika nyanja zote za Tunisia.

Ahadi ya Kudumu
Mkusanyiko wa kusimama kidete unaoandaliwa na wanaharakati wa Jumuiya ya “Wanaoiunga Mkono Palestina” mbele ya Ukumbi wa Manispaa katika mji mkuu wa Tunisia umeendelea kwa wiki 129 mfululizo, kwa sababu Watunisia wanasisitiza kwamba; mzingiro unaweza kuzingira watu, lakini hauwezi kuzingira dhamiri.

Katika kivuli cha vita vya mauaji ya kimbari vya Kizayuni ambavyo vimesababisha idadi ya kutisha ya waliouawa na waliojeruhiwa, sauti ya Tunisia inaendelea kusikika kwa nguvu ikilaani aina yoyote ya uzembe au kuafikiana na sera za ukaliaji wa mabavu zinazowazuia majeruhi wa Kipalestina kupata matibabu.

Mikusanyiko hii ya kusimama kidete ina umuhimu mkubwa wa kimkakati na wa kiishara kwa sababu nyingi, miongoni mwa sababu muhimu zaidi ni uimara wa mapambano, kwani kuendelea kwa maandamano kwa zaidi ya miaka miwili kunaonyesha kiwango cha juu cha mwamko wa wananchi wanaolichukulia suala la Ghaza kuwa suala la msingi lisiloweza kupuuzwa wala kuachwa.

Wanaharakati wanaamini kwamba; ukimya wa kimataifa kuhusu yale yanayotokea Ghaza ni aina ya ushiriki usio wa moja kwa moja katika jinai ya mzingiro wa kunyonga na kukandamiza maisha ya watu.

Mikusanyiko hii pia imekuwa sura ya mbele ya wananchi wa Tunisia ambao wanakataa aina yoyote ya kuafikiana na simulizi za Kizayuni na wanasisitiza kwamba; Ghaza ni sehemu isiyotenganishwa na undani wa utambulisho wa kitaifa wa Kiarabu.

“Mashujaa wa Muqawama”, Alama ya Changamoto

Sadiq Ammar, mmoja wa viongozi wa Jumuiya ya Wanaiounga Mkono Palestina na Rais wa Muungano wa Kitunisia wa Haki ya Palestina, katika mazungumzo na tovuti ya habari ya Al-Ahed, alieleza msimamo wa mitaa ya Tunisia kuhusu “Msafara wa Muqawama”, huku akisisitiza kwamba; hatua ya mashujaa hao kilikuwa kitendo kilichofichua maeneo dhaifu ya jamii ya kimataifa.

Ammar alisisitiza kwamba; mashujaa wa Msafara wa Muqawama waliikabili hujuma ya Kizayuni na wakafuata njia ya wapigania uhuru na watu huru.

Pia alizungumzia nafasi ya kiishara ya mapambano ya Izz al-Din al-Qassam na watu wote waliotoa maisha na mali zao muhanga, huku akiisifu Tunisia kwa msaada wake ambao umevuka kiwango cha mshikamano wa kawaida na kuwa ushiriki wa moja kwa moja katika juhudi za kuvunja mzingiro.

Alizitaja hujuma ya Kizayuni dhidi ya msafara huo kuwa fedheha mpya ya kimataifa na akabainisha kwamba; Watunisia hawatawasahau mashujaa wa Muqawama, wale waliothibitisha kwamba, kuvunja mzingiro kunawezekana ikiwa kutakuwepo nia thabiti.

Ammar alisisitiza kwamba; Muhammad Amir Bennour na wenzake ni alama ya irada ambayo hatimaye itapata uhuru, kama ilivyokuwa kwa mashujaa waliopata uhuru nchini Tunisia hapo awali.

Aliahidi tena kwamba; Tunisia haitaisahau Ghaza, na kwamba misafara inayotoka kwa lengo la kuvunja mzingiro ni kielelezo cha irada ya mataifa ambayo mwishowe yataushinda ujeuri na kiburi cha ukaliaji wa mabavu.

Kutokuwa na faida misimamo ya Kimataifa

Mateso ya watu wa Ghaza, ambako takriban Wapalestina milioni 1.5 wanaishi bila makazi baada ya nyumba zao kuharibiwa, ndiyo nguvu kuu inayochochea harakati hizi za mapambano.

Katika muktadha huo, Jumuiya ya “Wanaoiunga Mkono Palestina” imesisitiza kwamba; kuwazuia wagonjwa kutoka nje kwa ajili ya matibabu au kuwazuia mahujaji kutekeleza ibada ya Hija ni jinai ya wazi inayoongezwa katika orodha ndefu ya uhalifu wa wavamizi wa Kizayuni.

Watunisia wamethibitisha kwamba Palestina ni suala la heshima ya mwanadamu, wakati watu wa Ghaza wanaukabili mzingiro kwa subira yao, Watunisia wanaukabili kwa sauti zao zisizozimika, wakiuambia ulimwengu kwamba; “Msafara wa Muqawama” ulikuwa mshumaa uliowasha mwanga katikati ya giza la mzingiro na kufichua kutokuwa na faida misimamo dhaifu ya kimataifa.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha