Kwa mujibu wa Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, katika kipindi cha televisheni “Mashahidi Watoto wa Minab, Sauti ya Madhlumiyyah ya Umma” kilichorushwa Jumamosi tarehe 2 Dhul-Hijjah kwa juhudi za Majma‘ Al-Alami Qadimun kupitia kituo cha Al-Kawthar, Dkt. Abdul-Jabbar Al-Fahdawi, Mkuu wa Idara ya Baraza la Ribat Muhammadi la Iraq, alitoa hotuba iliyochambua jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya watoto na nafasi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kukabiliana na dhulma ya kimataifa.
Dkt. Al-Fahdawi, huku akitoa pongezi kwa kuwadia kwa siku za Idi Tukufu ya Adh-ha, alisema: “Katika siku hizi zenye baraka za mwezi wa Dhul-Hijjah, huku tukikaribia Idi ya Adh-ha, hatuna budi kuzungumzia yanayotokea katika zama hizi; kuhusu uasi wa dhulma, jeuri ya madhalimu na njama ambazo wakubwa wenye kiburi wamezifanya katika ardhi hii. Wanataka kutulazimisha kukubali mfumo huu wa Kimagharibi na Kimarekani, lakini kwa fadhila za baadhi ya nchi za Kiislamu, miongoni mwao Jamhuri ya Kiislamu, njama hii imefikia mwisho wake, Jamhuri ya Kiislamu ilisimama dhidi ya dhulma na ikasema: ‘Hapana dhulma, hapana uasi, hapana majabari.’”
Akirejelea mateso yanayotokana na Umma wa Kiislamu kuwa mbali na Mtume Mtukufu (saww) na njia yake ya kweli, aliongeza: “Leo hii Umma wa Kiislamu umekumbwa na kutawanyika na kuporomoka kutokana na utandawazi na mgawanyiko ambao utawala wa Kizayuni unaupanda ili kuimarisha uwepo wake katika ardhi za Kiislamu, Wazayuni wanadai haki ambayo si yao, huku wakisahau kwamba wanatekeleza ahadi ya Mwenyezi Mungu, ahadi ile ambayo Mwenyezi Mungu amesema:
﴿فَإِذَا جَاءَ وَعْدُ الْآخِرَةِ لِیَسُوءُوا وُجُوهَکُمْ وَلِیَدْخُلُوا الْمَسْجِدَ کَمَا دَخَلُوهُ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَلِیُتَبِّرُوا مَا عَلَوْا تَتْبِیرًا﴾.”
"Na ikifika ahadi ya mwisho ili waziharibu nyuso zenu, na waingie Msikitini kama walivyo ingia mara ya kwanza, na waharibu kila walicho kiteka kwa uharibifu mkubwa".
Mkuu wa Idara ya Baraza la Ribat Muhammadi la Iraq, akizungumzia jinai ya hivi karibuni katika shule ya Minab, alisema: “Jambo la mwisho walilofanya ni kuwaua watoto katika shule na kumwaga damu ndani ya nyumba za elimu na maarifa, kitendo hiki si jambo la kushangaza kwao, kama walivyofedheheka katika ‘Kisiwa cha Epstein’ kilicholaaniwa; mahali ambapo wanakunywa damu, wanawakatakata watoto vipande vipande na kufanya matendo yanayofanana na utekelezaji wa amri za Ibilisi, wao katika zama hizi ni mfano halisi wa dhulma na matendo ya Dajjali.”
Dkt. Abdul-Jabbar Al-Fahdawi, akipongeza uimara wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, alisema: “Jamhuri ya Kiislamu haijiwakilishi yenyewe tu, bali inawakilisha Umma mzima wa Kiislamu, maadui hawapingi jina la Jamhuri ya Kiislamu pekee, bali wanataka kuangamiza kila nguvu inayofuata Umma wa Muhammad (saww). Hawataki kabisa Umma wa mpenzi wa Mwenyezi Mungu wasimame tena.
Iwapo wanadai kwamba hawataki Jamhuri ya Kiislamu iwe na silaha za nyuklia ilhali nchi nyingi duniani zinazo silaha hizo, basi lengo lao la kweli ni kuangamiza dola yoyote ya Kiislamu; kwa sababu wanafahamu itikadi ya Umma wa Kiislamu iliyo katika Qur’ani na katika mwenendo wake, ambayo haikubali dhulma.”
Aliongeza kuwa: “Jamhuri ya Kiislamu imechukua msimamo mmoja unaofanana na msimamo wa Imam Hussein (as); msimamo wa watu wa heshima, ujasiri ambao Jamhuri ya Kiislamu imeuonesha na kuifanya dunia yote isimame kukabiliana na Marekani, nchi za Ulaya na Wazayuni, ni jambo la kustahili pongezi.
Leo hata katika duru za Ulaya inazungumzwa dhidi ya utawala wa Kizayuni, zamani watu waliogopa kuuawa, lakini leo Jamhuri ya Kiislamu imechora mstari mpya katika zama hizi na kuthibitisha kwamba; kuna zaidi ya msimamo mmoja na zaidi ya nguvu moja, na kwamba ni lazima kuwepo uwiano katika zama hizi.”
Mkuu wa Idara ya Baraza la Ribat Muhammadi la Iraq, mwishoni mwa hotuba yake, aliwashukuru waandaaji wa Majma‘ Al-Alami Qadimun na kusema: “Leo, kwa fadhila za Mola Mlezi, nguvu ni ya Waislamu na ni ya Uislamu, ninatoa shukrani na pongezi zangu zote kwa Taasisi ya Qadimun ambayo usiku na mchana inajitahidi kuandaa makongamano haya kupitia mtandao na kwa njia ya mikutano ya ana kwa ana, na inathibitisha ukweli huu kwa Umma wa Muhammad (saww) kwamba Umma huu bado unaishi.
Namuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu atutie nguvu katika ardhi hii kwa uwezo, ufahamu, ghera na elimu; na aurudishe ustaarabu huu wa Kiislamu katika utukufu wake wa zamani na katika uhalisia wetu wa kweli, kana kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) yuko miongoni mwetu.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu aendelee kutuneemesha kwa neema ya usalama, ushindi na kuwezeshwa; hakika yeye ni Mwenye kusikia na Mwenye kuitikia maombi.”
Maoni yako