Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Delpedro Marhaen, Mkurugenzi Mtendaji wa Lokataru Indonesia, pamoja na wanaharakati wengine wa kisiasa waliokuwa wamekamatwa kwa sababu ya kuunga mkono muqawama, waliinua bendera ya Iran kabla ya kuanza kwa kikao cha utoaji wa hukumu, Delpedro ni mmoja wa wanaharakati wa kisiasa na mtetezi wa wananchi wenye kudhulumiwa wa Palestina.
Inafaa kutajwa kuwa hapo awali Delpedro pamoja na wanaharakati wengine watatu wa kisiasa waliokuwa wamekamatwa wakati wa maandamano ya kupinga mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina yaliyofanywa na Israel mwishoni mwa Agosti 2025 nchini Indonesia, walikuwa wameachiliwa huru na jopo la majaji.
Pedro ambaye anajulikana kwa jina la utani la “Pedro”, ametangaza kuiunga mkono Iran na amelaani mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran, mashambulizi ambayo matokeo yake yalikuwa ni kuuawa kishahidi Ayatullah al-Udhma Sayyid Ali Khamenei.
“Sisi tunaiunga mkono Iran!” Pedro alitamka sentensi hii katika Mahakama ya Wilaya ya Kati ya Jakarta siku ya Ijumaa (6/3/2026).
Mbali na ujumbe unaohusiana na Iran, Pedro pia alitangaza uungaji mkono wake kwa uhuru wa Palestina na akamtaka Rais wa Indonesia, Prabowo Subianto, kuitoa Indonesia kutoka katika uanachama wa “Board of Peace”.
Alisisitiza kuwa: “Hususan kuhusiana na Palestina, sisi tunaiomba serikali ya Indonesia na Rais Prabowo Subianto kujiondoa kutoka Board of Peace na kuchukua msimamo katika kuunga mkono uhuru wa Palestina!”
Chanzo: Liputan6
Maoni yako