Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha Shirika la Habari la Hawza, maandamano hayo makubwa yalianza karibu na kituo cha metro cha Wilmersdorfer Strasse, ambapo umati mkubwa wa watu wanaopenda uhuru walikusanyika katika eneo hilo, kisha wakaandamana kuelekea katikati ya jiji huku wakipeperusha bendera za Palestine na kupaza sauti za kuiunga mkono Palestina.
Washiriki wa maandamano hayo walikuwa wamebeba mabango yenye ujumbe wa kutaka kusitishwa kwa mauaji ya kimbari huko Ghaza yanayofanywa na utawala wa Kizayuni unao mwaga damu, kulindwa kwa raia, kuhifadhiwa kwa utu wa kibinadamu na kusimamishwa mara moja kuuliwa kwa watoto.
Umati huo pia ulipaza kauli mbiu zikiwemo “Palestina iwe huru”, na waliutuhumu utawala wa Israel kwa kufanya mauaji ya makusudi na kuwalenga watoto. Katika baadhi ya kauli mbiu pia walimtaja Friedrich Merz, Kansela wa Germany, na wakakosoa msimamo wake kuhusu mzozo huo.
Maandamano hayo ya maelfu ya watu mjini Berlin ni sehemu ya wimbi kubwa zaidi la maandamano katika miji mbalimbali ya Ulaya, na upinzani wa wananchi dhidi ya vita vinavyoendelea na mauaji ya kimbari huko Ghaza.
Chanzo: EUPAC
Maoni yako