Jumamosi 9 Mei 2026 - 14:40
Makosa 14 ya kimahesabu aliyoyafanya adui katika vita vya kulazimishwa vya Ramadhani

Hawza/ Khatibu wa Swala ya Ijumaa wa Qum alielezea makosa 14 ya kimahesabu yaliyofanywa na adui katika vita vya Ramadhani, na kusisitiza kwamba; makosa hayo yamewaweka katika mashinikizo makubwa ya kimkakati.

Kwa mujibu wa wa Shirika la Habari la Hawza, Alireza Arafi katika hotuba za Swala ya Ijumaa ya tarehe 18 Ordibehesht 1405 Hijria Shamsia (8 May 2026) zilizofanyika katika Muswalla Quds mjini Qom Iran alisema: “Maadui katika tathmini yao kuhusu Iran na Muqawama walifanya makosa kadhaa ya kimahesabu, na makosa hayo yamewaweka katika mashinikizo makubwa na ya kimkakati.”

Imamu wa Ijumaa wa Qum aliendelea kusema: “Miongoni mwa makosa yao ni kwamba; walikuwa wanategemea tu hesabu na nadharia za elimu zao za siasa na sayansi za kibinadamu, huku wakipuuza mambo mengine. Hawakuielewa mantiki ya Ashura na Uislamu, wala hawakuzingatia kwa makini saikolojia na sosholojia ya taifa la Iran; ndio maana wakaangukia katika tathmini potofu.”

Khatibu wa Swala ya Ijumaa wa Qum huku akibainisha kuwa; mwanzo wa kuanguka kwa jeshi lolote vitani ni kufanya tathmini mbaya kuhusu upande wa pili, alielezea vipengele vingine vya makosa ya kimahesabu ya adui:

Makosa katika tathmini kuhusu uwepo wa wananchi uwanjani;

Makosa katika tathmini kuhusu machafuko ya mitaani na fitna;

Makosa kuhusu kusambaratika kwa mfumo wa kisiasa na vyombo vya dola;

Makosa katika tathmini ya mbinu ya kujihami ya Iran (kwamba Iran itaendelea kujihami kwa mtindo wa zamani);

Makosa kuhusu mhimili wa Muqawama;

Makosa kuhusu uungaji mkono wa kimataifa;

Makosa kuhusu mantiki ya kidini ya Iran.

Makosa 7 ya Wamarekani katika kujitathmini wenyewe

Kosa la kwanza: Tathmini potofu kuhusu wanafiki na maadui wa Iran

Imamu wa Ijumaa wa Qum alisema: “Adui ilifanya kosa kuhusu wanafiki, mamluki na wenye chuki wa Kiirani walioko upande wao. Walimchukulia kuwa mtoto mkubwa aliyezaliwa katika familia yenye nuksi ya Pahlavi pamoja na vibaraka wengine kama yeye, na wakadhani kwamba iwapo jambo lolote lingetokea, wangekuwa jeshi litakalobadilisha mlinganyo.”

Aliendelea kusema: “Walifanya kosa kuhusu mamluki hawa ambao wengi wao wako nje ya nchi na hawana uelewa wowote kuhusu jamii ya Iran. Hili kundi dogo la waoga, wanaodai mengi bila uwezo na waliokata tamaa, lilififia mbele ya Wairan wengi. Hata mbele ya Wairani waishio nje ya nchi walibaki wachache, na Wairani wa nje ya nchi walionesha mshikamano na Iran zaidi ya matarajio ya maadui.”

Kosa la pili: Tathmini potofu kuhusu makundi ya wanaotaka kujitenga

Mkurugenzi wa Hawza alisema: “Walikuwa wameweka matumaini yao kwa makundi ya kikabila yanayotaka kujitenga, wakidhani kuwa baadhi ya makundi madogo yaliyopotoka yangekuwa mtaji wao na yangekuwa na nafasi muhimu katika vita vya ardhini. Hili lilikuwa kosa, kwa sababu taifa la Iran ni moja; makabila mbalimbali na madhehebu tofauti ni sehemu ya mwili mmoja na ni pete za mnyororo imara.”

Kosa la tatu: Tathmini potofu kuhusu washiriki wao wa Ulaya

Imamu wa Ijumaa wa Qum huku akibainisha kuwa; adui hata kuhusu washirika wake hakuwa na tathmini sahihi, alisema: “Adui ilifanya hesabu mbaya kuhusu Ulaya na washirika wake. Ulaya imekwama katika vita vya Ukraine, na imeathirika katika suala la nishati na maslahi yake. Hata Donald Trump mwenyewe alisema kuwa; wao wanatutegemea. Barani Ulaya baadhi walichukua misimamo mizuri kiasi, na hata maadui na wapinzani hawakuwa na uwezo wa kuandamana na mashambulizi ya kijeshi.”

Kosa la nne: Tathmini potofu kuhusu nchi za eneo

Mjumbe wa mafakihi wa Baraza la Kulinda Katiba alisema: “Katika eneo hili baadhi ya nchi zilifikiria kwa usahihi na zikajiepusha; japokuwa hatua sahihi na ya busara zaidi ilikuwa ni kusimama dhidi ya waporaji katika ulimwengu wa Kiislamu.”

Mkurugenzi wa Hawza alisema: “Adui ilidhani kwamba; baadhi ya tawala tegemezi za Ghuba ya Uajemi ambazo ziko dhaifu mbele yake zinaweza kufanya jambo fulani, ilhali hata zimeshindwa kulinda vituo na maslahi ya adui.”

Alisema: “Leo taifa kubwa la Iran linaziambia serikali za kandokando ya Ghuba ya Uajemi: simameni pamoja na Uislamu, Palestina na mataifa yenu, simameni upande wa Iran. Iran itakuwa rafiki mwema na mwaminifu kwenu, Iran ni mwamba mgumu, safu ya chuma, mhimili wa Muqawama na jihadi; msisimame dhidi yake.”

Kosa la tano: Dhana potofu kuhusu China na Urusi

Imamu wa Ijumaa wa Qum alisema: “Adui ilidhani kuwa China na Urusi zingejiondoa kimya kimya. Ni kweli kwamba sisi katika jihadi yetu hatujawahi kumtegemea yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu, wala hatukumfanya yeyote isipokuwa Yeye kuwa msingi wa nguvu zetu; lakini China na Urusi zilipinga azimio hilo kwa kura ya veto na hazikushirikiana nanyi.”

Kosa la sita: Tathmini isiyo sahihi kuhusu jeshi lao wenyewe

Alisema: “Adui alikuwa imeweka matumaini makubwa kwa manowari kubwa, ndege za kisasa na mbinu zilizojaribiwa. Donald Trump alikuwa anaamini kuwa; jeshi la Marekani ndilo lenye nguvu zaidi duniani. Kiongozi wetu shahidi alisema kuwa, nguvu ya Mwenyezi Mungu iko juu yao. Hivyo ndivyo manowari za adui zilivyolazimika kujificha, ndege zao zikaanguka na mifumo yao ya ulinzi ikasambaratika.”

Kosa la saba: Kutegemea mno utawala wa Kizayuni

Khatibu wa Sala ya Ijumaa wa Qum aliendelea kusema: “Adui iliuchukulia utawala haram wa Israel kuwa ni jambo muhimu, na utawala huo haram ulikuwa kila mara ukiidanganya Marekani kwamba iingie katika mapambano haya na kwamba wao watatoa pigo la mwisho. Nyinyi hata Israel yenu hamkuijua vizuri.”

Mjumbe wa mafakihi wa Baraza la Kulinda Katiba akiwaelekea maadui alisema: “Makosa saba ya kimahesabu katika kuitathmini Iran na makosa saba ya kimahesabu katika kujitathmini nyinyi wenyewe yamesababisha kushindwa kwenu.”

Nasaha kwa taifa

Alireza Arafi aliendelea kusema: “Sisi tuko katikati ya mapambano makubwa, na lazima tuwe na maandalizi muhimu:

1- Kuvumilia matatizo;

2- Kuendelea kuwepo katika medani;

3- Kushirikiana na viongozi wa serikali katika kudhibiti bei na masuala ya uchumi;

4- Kushirikiana na kujitahidi katika kujenga upya na kurekebisha madhara ya kipindi cha vita;

5- Kujiandaa kwa kipindi cha baada ya vita na kwa vita vyenyewe.”

Mkurugenzi wa Hawza za elimu za dini nchini alisisitiza: “Dunia lazima ijue kuwa taifa la Iran bado liko tayari kuendeleza vita na kumuangamiza adui, na liko katikati ya medani.”

Majukumu ya viongozi

Alireza Arafi aliendelea kutaja majukumu muhimu zaidi ya viongozi:

Kuendelea kuwahudumia wananchi kwa kujiamini na kusisitiza uwezo wa ndani;

Kutafuta suluhisho za matatizo;

Kuzingatia na kuipa umuhimu uchumi wa kujitegemea na kaulimbiu ya mwaka;

Kukataa uchumi wa kibepari wa Magharibi na nadharia tegemezi; tuweke msingi wa uchumi unaotegemea wananchi kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu na watu;

Kuwa makini katika mazungumzo na mijadala;

Kujiandaa kwa chaguo zote na hali zote zinazoweza kutokea.


Imamu wa Ijumaa wa Qum alisema: “Mara nyingi tumepigwa na maadui na wamefanya khiyana. Lazima tuwe waangalifu na wenye umakini. Zamani tulikuwa tunalegeza misimamo ili vita visitokee, lakini sasa tumeshapita hatua hiyo.”

Alisema: “Tumeonyesha kuwa vita vya kulazimishwa haviwezi kuliangusha taifa hili kubwa na mhimili wa Muqawama. Ni lazima kusimama imara na kujiandaa kwa chaguo zote. Tuwe na yakini kwamba kwa kufuata uongozi, mshikamano, umoja, jihadi na juhudi za kuendeleza uwezo wa kijeshi tunaweza kuendelea na njia yetu.”

Khatibu wa Sala ya Ijumaa wa Qum akiupongeza Wiki ya Kazi na Wafanyakazi pamoja na kuwakumbuka mashahidi wa sekta hiyo alisema: “Ninawashukuru wafanyakazi wote, wawekezaji na wanaharakati wa sekta ya uchumi, hususan wale walioathirika katika vita lakini bado wamesimama kwa ajili ya maendeleo ya uchumi na viwanda.”

Akiashiria Wiki ya Elimu na Malezi alisema: “Furaha ya dunia na Akhera ya kizazi kijacho iko katika mfumo madhubuti wa elimu na malezi wenye heshima na uliojengwa juu ya fikra za Mwenyezi Mungu. Fikra ambazo misingi yake imechorwa katika hati ya mageuzi ya elimu na malezi.”

Heshima ni miongoni mwa nguzo za utambulisho wa jamii ya Kiislamu

Alireza Arafi katika khutba ya kwanza kuhusu heshima ya Kiislamu alisema: “Heshima ni miongoni mwa nguzo za msingi za jamii ya waumini, ya kimungu na ya tawhidi. Mtu muumini ana heshima, jamii ya waumini na ya Kiislamu ina heshima, utukufu na adhama ya ndani.”

Imamu wa Ijumaa wa Qum huku akisisitiza kwamba, kipengele cha heshima ni miongoni mwa nguzo za utambulisho wa jamii ya Kiislamu alisema: “Iwapo jamii inataka kuwa ya Kiislamu, basi kipengele cha heshima, utu na sharafu lazima kionekane ndani yake.”

Mjumbe wa Baraza la Wataalamu wa Uongozi huku akibainisha kuwa, watu wa Iran wameonesha mifano ya juu zaidi ya heshima ya Kiislamu mbele ya dunia alisema: “Watu watukufu wa Iran katika miongo kadhaa wameonesha heshima hii, utu huu na sharafu hii ya kiimani. Bado tunapaswa kuulinda utambulisho huu wa heshima, sharafu na uimara, kwa sababu siri ya maendeleo na ustawi imo katika kipengele cha heshima ya Kiislamu na kuikuza ndani ya jamii.”

Mkurugenzi wa Hawza alisisitiza: “Mfumo wa elimu na malezi, mfumo wa kisiasa na mfumo wa familia vinapaswa kuwa namna ya kumlea mtoto kwa heshima.”

Akiwa amesema kuwa heshima maana yake ni kutoshindikika kunakotokana na hisia ya adhama, utukufu, nguvu na kutokuyumbishwa, alisema: “Heshima imegawanyika katika viwango viwili: kiwango cha mtu binafsi na kiwango cha kijamii. Katika kiwango cha mtu binafsi ni kujithamini, lakini katika kiwango cha juu cha kijamii ni heshima ya ustaarabu, ambayo ni kipengele cha msingi katika haiba ya kijamii ya jamii ya Kiislamu.”

Khatibu wa Swala ya Ijumaa wa Qum aliendelea kusema: “Katika Qur’ani Tukufu, Mwenyezi Mungu ametajwa kwa sifa ya Mwenye nguvu na heshima zaidi ya mara 90, na aya kadhaa zimeashiria vipengele vya kijamii na kuzungumzia kudhihiri kwa heshima ya Mwenyezi Mungu ndani ya jamii ya Kiislamu.”

Akiweka mkazo kwamba jamii ya Kiislamu ni jamii ambayo ni kioo cha heshima ya Mwenyezi Mungu alisema: “Mwenyezi Mungu katika aya ya 10 ya Suratul Fatir anasema:


Mwenye kutaka heshima, basi heshima yote ni ya Mwenyezi Mungu.»”

Imamu wa Ijumaa wa Qum akirejea aya ya 139 ya Suratun Nisaa: alisema:

“Wanafiki ni wale wanaotafuta heshima kwa makafiri, na wanaitafuta kwa kujisalimisha mbele yao, ilhali heshima yote ni ya Mwenyezi Mungu, na kama mnataka heshima basi hakuna isipokuwa katika uwepo wa Mwenyezi Mungu.”

Alireza Arafi akirejea aya ya 69 ya Suratu Yunus alisema:

“Mwenyezi Mungu katika aya hii anasema msiogope kejeli na lawama za wengine, kwa sababu heshima zote ziko kwa Mwenyezi Mungu. Inawezekana tarumbeta zao za vyombo vya habari zikakuhuzunisha, lakini kamwe msiogope.”

Mkurugenzi wa Hawza huku akisisitiza kwamba, taifa la Iran limeigusa na kuidhihirisha kwa vitendo elementi hii ya kiimani na utambulisho wa Kiislamu yaani heshima, aliongeza: “Mwenyezi Mungu katika aya ya 8 ya Suratul Munafiqun anasema: «وَلِلَّهِ الْعِزَّةُ وَلِرَسُولِهِ وَلِلْمُؤْمِنِینَ». Aya hii inaeleza mwendelezo wa heshima ya Mwenyezi Mungu kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) na baada yake kwa jamii ya Kiislamu.”

Nguzo za heshima

Nguzo ya kwanza: Fikra na mawazo

Alireza Arafi alisema: “Nguzo ya kwanza ya kufanikisha heshima katika kiwango cha kijamii na kiustaarabu inahusiana na ulimwengu wa ndani wa nafsi zetu. Jamii ambayo ndani yake imejaa kumtambua Mwenyezi Mungu, kujitambua, uelewa na kujiamini huwa ni jamii yenye heshima.”

Khatibu wa Swala ya Ijumaa wa Qum alisisitiza: “Imamu muasisi wa Mapinduzi na kiongozi shahidi wa Mapinduzi katika miaka yote walisisitiza kujitegemea, kujiamini kitaifa na kujiamini binafsi. Ikiwa jamii itaisahau adhama ya Mwenyezi Mungu na mitaji yake ya ndani haitakuwa na heshima.”

Nguzo ya pili: Hamasa na azma madhubuti ya ndani

Mkurugenzi wa Hawza alisema: “Wakati mwingine mwanadamu anajua na kuelewa mambo lakini hasimami imara kwa irada madhubuti. Irada yenye nguvu, azma thabiti na uimara katika maamuzi ni nguzo ya pili katika heshima ya Mwenyezi Mungu.”

Nguzo ya tatu: Kutekeleza kwa vitendo

Alireza Arafi alisema: “Fikra, mawazo na irada madhubuti lazima vionekane katika vitendo na mwenendo, na vielelezo vya kujitolea, kujitoa muhanga, kusimama imara na uthabiti vionekane katika maisha ya kisiasa na kijamii.”

Alireza Arafi alisisitiza: “Iwapo jamii itakuwa na fikra na uelewa unaotegemea heshima, ikawa na irada na azma inayolenga heshima na utukufu, na katika vitendo na mwenendo wa maisha ya kijamii ikaishi kwa heshima na uimara, basi itageuka kuwa jamii ambayo waumini wake watakuwa mfano wa:

Mkurugenzi huyu wa Hawza alikumbusha kuww: “Msingi huu wa heshima ya Mwenyezi Mungu ukijikita ndani ya akili na dhamira ya jamii, basi utaonekana katika nguvu ya kielimu, kijeshi, kitamaduni, kiteknolojia, kiusalama, kisiasa, kiutawala na kidiplomasia. Ikiwa waumini wenye heshima na wanaonufaika na mwanga wa heshima ya Mwenyezi Mungu watakuwepo katika medani hizi, basi watakuwa viongozi wenye uimara na heshima.”

Mjumbe wa mafakihi wa Baraza la Kulinda Katiba aliendelea kusema: “Katika historia ya miaka 200 iliyopita ya Iran, mara nyingi kutokana na khiyana za watawala na udhaifu wa watu, heshima yetu iliporwa. Historia hii vijana na jamii yetu wanapaswa kuijua. Katika Vita vya Kwanza na vya Pili vya Dunia tulitangaza kutokuwa upande wowote, lakini kwa sababu ya kukosekana heshima ya Kiislamu walituvamia na kuwatupa viongozi wa nchi kama taka.”

Imamu wa Ijumaa wa Qum aliongeza: “Katika nyaraka zilizochapishwa za Waingereza kuhusu mkataba wa mwaka 1919 wa Wuthuqud-Dawla, ambao shahidi Sayyid Hassan Modarres alisimama peke yake dhidi yake, imekuja kwamba Ahmad Shah, Wuthuqud-Dawla na Nusratud-Dawla walisema: ‘Tunasaini mkataba huu ili mtupe mishahara.’ Mfalme wa Iran alikuwa amejisalimisha kwa wageni na alikuwa anasaini mikataba ya kikoloni ili apate mshahara.”

Alireza Arafi mwishoni alisisitiza: “Mapinduzi ya Kiislamu yalileta mabadiliko haya na yakafufua heshima ambayo mara nyingi ilikuwa imekandamizwa, na yakabadilisha mlinganyo wa dunia. Leo sisi tumekuwa wenye athari katika mlinganyo wa dunia. Tuko katikati ya mapambano ya kihistoria na ya kiustaarabu, na lazima tuilinde heshima hii.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha