Jumatatu 20 Aprili 2026 - 02:20
Kusimama kidete kwa Iran na uthabiti wa Hizbullah kuliilazimisha Marekani na Israel kukubali usitishaji wa mapigano

Hawza/ Ayatullah Sayyid Yasin Mousawi alisisitiza kuwa; msimamo thabiti wa kimkakati wa Iran pamoja na ustahimilivu wa kijeshi wa Hezbullah, uliibadilisha mizania kwa manufaa ya muqawama na kuilazimisha Marekani na utawala wa Kizayuni kukubali usitishaji wa mapigano.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Sayyid Yasin Mousawi, Imamu wa Swala ya Ijumaa wa Baghdad na mmoja wa walimu mashuhuri wa Hawza ya Najaf, katika khutba za Swala ya Ijumaa, huku akirejelea masuala mbalimbali ya kisiasa, kiuchumi na maendeleo ya kikanda, alichambua changamoto zinazoikabili Iraq na hali ya eneo kwa ujumla.

Akiashiria kuwa mgogoro wa kisiasa nchini Iraq bado unazunguka namna ya utekelezaji wa katiba, hasa katika suala la uchaguzi wa rais na uundaji wa serikali, alisema: wananchi wa Iraq walishiriki katika uchaguzi na kupiga kura zao, lakini mivutano ya kisiasa, hasa kati ya makundi ya Kikurdi, ilizuia kwa muda mrefu utekelezaji wa haki za kikatiba.

Ayatullah Mousawi aliongeza kuwa: uchaguzi wa hivi karibuni wa rais hatimaye ulifanyika kwa makubaliano ya kisiasa, lakini mchakato huu unakosolewa, kwa sababu kigezo cha uchaguzi kilikuwa zaidi chini ya maslahi ya vyama kuliko uadilifu na sifa stahiki. Kwa mujibu wake, mara nyingi makundi ya kisiasa hufikia muafaka juu ya chaguo fulani bila kuzingatia ni nani anayefaa zaidi kuiwakilisha nchi.

Aliendelea huku akionya kuhusu suala la uchaguzi wa waziri mkuu: kurudiwa kwa mtindo huo huo katika uteuzi wa mkuu wa serikali kutasababisha “kosa jipya la kisiasa”. Kuweka mipaka ya chaguo katika duara finyu la watu ni dalili ya kutanguliza maslahi ya vyama juu ya maslahi ya taifa.

Imamu wa Swala ya Ijumaa wa Baghdad alisisitiza ulazima wa kuchagua shakhsia huru na yenye ufanisi, na akasema: uwaziri mkuu ni haki ya taifa, siyo fursa ya vyama. Pia alivitaka vyama vya kisiasa katika kupendekeza mgombea wa nafasi hiyo kuzingatia vigezo vya uhalisia zaidi na kutoweka mipaka kwa majina machache tu.

Ayatullah Mousawi pia aligusia maendeleo ya Lebanon na kwa kukosoa baadhi ya misimamo ya kisiasa katika nchi hiyo alisema: kupinga kuunganisha usitishaji wa mapigano na mchakato wa mazungumzo kati ya Iran na Marekani kwa upatanishi wa Pakistan kulisababisha kuongezeka kwa mapigano na vifo vya mamia ya raia wasio na hatia.

Alisisitiza kuwa: maendeleo ya hivi karibuni, ikiwa ni pamoja na tangazo la usitishaji wa mapigano, ni matokeo ya shinikizo na misimamo ya Iran pamoja na muqawama wa kijeshi wa Hezbullah, na kwamba “muqawama” ndiyo uliokuwa sababu kuu katika kulazimisha hali hizi kwa upande wa pili, siyo tu mchakato wa kidiplomasia.

Imamu wa Swala ya Ijumaa wa Baghdad aliongeza: yaliyotokea Lebanon yanaonesha umuhimu wa kushikamana na chaguo la muqawama mbele ya changamoto. Aliyataja mataifa ya eneo hilo, hasa nchi za Ghuba ya Uajemi, na kuyataka kuimarisha ushirikiano wa kikanda, kuepuka kutegemea nguvu za nje, na kuchukua hatua kuelekea kuondolewa kwa kambi za kigeni katika eneo hilo.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha