Jumanne 14 Aprili 2026 - 10:20
Watu wa Urusi waliandika nini katika daftari la kumbukumbu la mshikamano na Iran?

Hawza/ Sambamba na kufanyika kwa maonyesho ya ishirini na sita ya fasihi ya fikra na isiyo ya kubuni (Non-fiction) ya Urusi mjini Moscow, banda la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran liligeuka kuwa uwanja wa kuonesha mshikamano wa kitamaduni na wa wananchi; mahali ambapo washiriki wakirusi kwa kuandika ujumbe wa kuliunga mkono taifa la Iran na kwa kushiriki katika hafla ya uzinduzi wa kazi mpya, walionesha uhusiano wa kitamaduni na kibinadamu kati ya mataifa hayo mawili.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, maonyesho ya ishirini na sita ya fasihi ya fikra na isiyo ya kubuni (Non-fiction) ya Urusi yamefanyika kuanzia tarehe 9 hadi 12 Aprili 2026 (21 hadi 24 Farvardin 1405) katika kituo cha Gostiny Dvor mjini Moscow.

Wageni wa toleo la ishirini na sita la maonyesho ya fasihi ya fikra (Non-fiction) ya Urusi, kwa kuhudhuria katika banda la Iran na kuandika ujumbe katika daftari la kumbukumbu, walisisitiza kwamba, daima wamesimama pamoja na watu wa Iran.

Iran iendelee kuwepo!
Salamu kwa Wairani mashujaa!
[Iran] ni mfano kwetu na kwa wote!
Iran ni tumaini la ubinadamu!

Ni miongoni mwa kauli mbiu ambazo zilionekana katika maandishi mengi ya Warusi waliotembelea banda la Iran katika maonyesho hayo.

Katika maonyesho hayo, wasifu wa maisha wa kiongozi wa tatu wa Mapinduzi, Mtukufu Ayatollah Sayyid Mujtaba Husseini Khamenei (Mola amlinde), umezinduliwa kwa lugha ya Kirusi katika jarida lenye anwani “Kiongozi wa Tatu” katika banda la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika maonyesho ya vitabu ya Moscow.

Katika hafla hiyo ambayo ilifanyika kwa mnasaba wa siku ya arubaini tangia kuuawa kishahidi Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, balozi wa nchi ya Iran mjini Moscow pia alizindua kitabu chenye anuani isemayo “Baba Mwenye Huruma” kwa lugha ya Kirusi, ambacho kina simulizi kuhusu maisha ya kiongozi shahidi wa Mapinduzi.

Kazem Jalali, Balozi wa Iran nchini Urusi, baada ya uzinduzi wa kazi hizi, pamoja na kutoa shukrani kwa kasi ya utendaji ya Shirika la Utamaduni na Mawasiliano ya Kiislamu na shirika la uchapishaji la kimataifa la Nakhl Sabz katika kuandaa kitabu “Baba Mwenye Huruma” baada ya kuuawa kishahidi kiongozi mkuu wa Mapinduzi, alikitaja kitabu hiki kuwa ni kazi yenye thamani kwa ajili ya kumtambulisha Ayatullah Sayyid Ali Khamenei kwa wazungumzaji wa Kirusi.

Mshikamano wa watu wa Urusi na Iran

Pia kitabu “Siku 12”, ambacho ni simulizi ya nguvu na kudhulumiwa kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kukabiliana na uvamizi wa Marekani na Uzayuni katika vita ya siku 12 (23 Khordad hadi 3 Tir 1404), nacho kilizinduliwa kwa lugha ya Kirusi. Katika maonyesho haya ya kimataifa, pia banda la uchapishaji la Sadra, linalohusiana na Taasisi ya Kiirani ya Tafiti za Kiislamu Ibn Sina iliyoko Moscow, limewasilisha vitabu vitatu vipya vilivyo na mada mbalimbali kutoka katika hotuba za Ayatullah Sayyid Ali Khamenei vyenye anuani “Imani”, “Mwanamke na Familia” na “Ndoa na Uchaguzi wa Mwenza” mbele ya hadhira.

Watu wa Urusi waliandika nini katika daftari la kumbukumbu la mshikamano na Iran?

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha