Jumatano 1 Aprili 2026 - 00:30
Watu wa Iran katika “Vita vya Ramadhani” kwa kuiga kielelezo cha Karbala wamesimama imara, wanatoa mashahidi na wanashinda kwenye vita

Hawza/ Ayatullah Sayyid Muhammad Taqi Mudarrisi amesema kuwa; watu wa Iran katika Vita vya Ramadhani wamepewa msukumo na roho ya Karbala iliyoakisiwa katika kujitolea kwa Imam Hussein (a.s.). Ndiyo sababu wanasimama dhidi ya nguvu kubwa zaidi za kibeberu, wanatoa mashahidi kwenye njia ya Mwenyezi Mungu, na wameshinda vita.

Kwa mujibu wa kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Sayyid Muhammad Taqi Mudarrisi katika darsa lake la wiki hii kwa wanafunzi wa hawza huko Karbala alisisitiza kwamba; mataifa ya Kiislamu, hususan watu wa Iran, wamemfanya Imam Hussein (a.s.), kuwa kielelezo katika maadili na katika misimamo yao. Kwa sababu hiyo waliinuka, wakajitoa muhanga, wakasimama imara na wakapata ushindi—hali ya kuwa nchi hiyo hapo awali ilihesabiwa miongoni mwa nchi zilizopo katika ulimwengu wa Tatu.

Aliongeza kusema: Kauli mbiu ambayo watu wa Iran waliitoa katika vita vyao dhidi ya Marekani na Israel inaonesha dhamiri, mabadiliko na ikhlasi yao; wao wanapaza sauti wakisema: “Hussein ni kauli mbiu yetu, shahada ni fahari kwetu.”

Ayatullah Mudarrisi alisisitiza kwamba; historia itarekodi simulizi ya kusimama kwa mataifa yetu dhidi ya ubeberu duniani hali ya kuwa mataifa mengi hayakuweza kustahimili au kufanya jambo hilo.

Mwalimu huyu mashuhuri wa Hawza aliuhesabu ushindi wa taifa la Kiislamu mbele ya nguvu kubwa ya kibeberu kuwa ni matokeo ya “kuhuishwa kwa roho”; roho inayochochea nguvu, inashughulikia mambo ya msingi, na kuyaweka pembeni mambo ya ziada na ya daraja ya pili yanayofunga azma na kuzuia kukabiliana na maadui.

Katika kufafanua hoja hiyo amesema: Mataifa yetu yamepata uhai tena; roho ya imani imefufuka ndani yao, na roho hii ndio uhai na kiini cha kila kitu. Roho ya swala ni kuuelekeza moyo kwa Mwenyezi Mungu na kukumbuka utukufu Wake, siyo tu mkusanyiko wa harakati zisizo na uhai. Roho ya elimu na fiqhi ni uelewa wa kina, si kuhifadhi maneno juu juu bila kuyaelewa. Kila jambo lina roho na kiini chake. Ni lazima tufike kwenye hiyo roho ambayo ndiyo hakika yake; yaliyo mengine ni ganda tu linaloilinda hiyo roho.

Mwishoni, Ayatullah Mudarrisi akabainisha: Tunapowaelekeza watu kwenye roho; roho ya fiqhi, roho ya swala, roho ya dini na roho ya jihad ndipo tutakapofanikiwa, tutakapotawala ulimwengu, na tutakapoleta amani na uadilifu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha