Jumapili 22 Machi 2026 - 20:00
Nimepokea kwa huzuni kubwa kuuawa kishahidi Dkt. Ali Larijani

Hawza/ Mustafa Şentop, Spika wa Bunge la Uturuki, kufuatia kuuawa kishahidi Dkt. Ali Larijani katika mashambulizi yiyofanywa na Marekani na Israel, katika ujumbe wake huku akionesha masikitiko yake kutokana na msiba huo, pamoja na kurejelea historia ya ushirikiano wa pamoja, alimtaja kuwa mwanasiasa mashuhuri aliyekuwa na nafasi ya pekee miongoni mwa taifa la Iran kutokana na misimamo yake thabiti dhidi ya mashambulizi hayo.

Kwa mujibu wa kitengo cha kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, kufuatia kuuawa kishahidi Dkt. Ali Larijani, Mustafa Şentop, Spika wa Bunge la Uturuki, alichapisha ujumbe katika akaunti yake rasmi ya X kama ifuatavyo:

“Nimepokea kwa huzuni kubwa taarifa ya kuuawa kishahidi kwa Dkt. Ali Larijani, Spika wa zamani wa Bunge la Jamhuribya Kiislamu ya Iran.

Bwana Larijani, ambaye wakati wa uongozi wetu wa pamoja katika mabunge yetu tulipata fursa ya kushirikiana naye kwa karibu, alikuwa mtu mashuhuri na mwanasiasa mwenye thamani aliyefahamika kwa utulivu na elimu yake.

Namwomba Mwenyezi Mungu amrehemu Bwana Larijani ambaye alisimama kwa heshima mbele ya mashambulizi yasiyo halali na yasiyo ya kiungwana ya Marekani na Israel, na ambaye alipata nafasi katika nyoyo za taifa la Iran, na ninatoa pole kwa familia yake na taifa ndugu la Iran.”

Nimepokea kwa huzuni kubwa kuuawa kishahidi Dkt. Ali Larijani

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha