Ijumaa 20 Machi 2026 - 21:10
Kuilinda Heshima ya Umma wa Kiislamu na Damu Safi ya Viongozi wa Kidini ni Wajibu wa Kimungu

Hawza/ Wanazuoni wa ahlu Sunna wa Iran, katika barua waliyoituma kwa wanazuoni na taasisi kubwa za Kiislamu duniani, wamesema kuwa; kuilinda heshima ya umma wa Kiislamu na damu safi ya viongozi wa kidini ni wajibu wa kimungu, na umoja wa wanazuoni unaweza kuwa ngome imara dhidi ya njama za maadui wa Uislamu.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, kundi la wanazuoni wa Kisuni wa Iran, kwa muktadha wa sikukuu ya Eid al-Fitr, katika barua yao kwa wanazuoni na taasisi mbalimbali kubwa za Kiislamu, ikiwa ni pamoja na Al-Azhar, Shirikisho la Wanazuoni wa Kiislamu, Jumuiya ya Fiqh ya Kiislamu, wanazuoni wa Saudi Arabia, Uturuki, Indonesia, Malaysia, Lebanon, Iraq, na Algeria, wamekemea vikali shambulizi la hivi karibuni la Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran na shahada ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Katika barua hiyo, imesema:

"Kitendo hiki cha kikatili si tu shambulizi kwa taifa la Iran, bali ni dhihaka ya wazi kwa heshima ya umma wa Muhammad (s.a.w) na thamani za kidini za Uislamu Mtukufu."

Wanazuoni wa ahlu sunna wa Iran, waliziomba taasisi za kidini katika ulimwengu wa Kiislamu, wakiwemo viongozi wa kidini na jumuiya za wanazuoni, kutoa msimamo wa pamoja na thabiti, kukemea uhalifu huu, na kutoa fatwa ya jihad dhidi ya utawala wa Kizayuni na ubeberu wa kimataifa.

Barua hiyo ilisisitiza kuwa: "Kulinda heshima ya umma wa Kiislamu na damu safi ya viongozi wa kidini ni wajibu wa kimungu, na umoja wa wanazuoni unaweza kuwa ngome imara dhidi ya njama za maadui wa Uislamu."

Mwisho wa barua hiyo, wanazuoni walimuomba Mwenyezi Mungu aunganishe mioyo ya waumini, aimarishe umma wa Kiislamu katika njia ya haki, na awadhalilishe madhalimu duniani.

Kuilinda Heshima ya Umma wa Kiislamu na Damu Safi ya Viongozi wa Kidini ni Wajibu wa Kimungu

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha