Kwa mujibu wa mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Qudsi leo yamefanyika katika mji mtakatifu wa Qum Iran na katika ardhi ya Karima wa Ahlul-Bayt (amani iwe juu yake), huku watu wa mapinduzi wakiwa katika huzuni na maombolezo ya kuuawa kishahidi kwa Kiongozi mkuu wa Umma, Ayatullah al-Udhma Imam Khamenei mpendwa, pamoja na mashahidi wa vita vilivyolazimishwa na Marekani na Uzayuni, hususan wanafunzi wanyonge wa Shule ya Shajarah Tayyibah ya Minab, ambao waliuawa kikatili na watu waovu zaidi duniani.
Wamekuja ili wasije wakamfedhehesha Kiongozi wao mkuu
Wananchi waaminifu wa Qum kabla ya kuanza rasmi kwa maandamano walielekea katika Haram tukufu ya Bibi Fatima Ma’sumah (amani iwe juu yake) ili waweze kuitikia wito wa Walii wa Amri na kutekeleza wajibu wao wa kidini, kimapinduzi na kitaifa, na ili wasije wakamuacha katika fedheha Sayyid al-Shuhadaa wa Mapinduzi ya Kiislamu na mashahidi wapendwa.
Maandamano ya kuvunja nguvu za maadui ya Siku ya Qudsi mwaka huu yameanza kwa ushiriki mkubwa na wa hamasa wa watu wa Qum, wakipaza sauti za:
“Allahu Akbar”,
“Kifo kwa Marekani”,
“Kifo kwa Israel”,
“Damu iliyo katika mishipa yetu ni zawadi kwa kiongozi wetu”,
“Sisi ni wadai wa damu ya kiongozi wetu, hatutasamehe Marekani”,
na kauli nyinginezo, huku mvua ikinyesha na maandamano yakianzia katika Haram tukufu ya Bibi wa Karama.
Vitisho navyo havikufua dafu
Njia zinazoelekea katika Haram tukufu zilijaa umati mkubwa wa watu ambao licha ya vitisho vya maadui wamesimama kwa uthabiti, kwa azma na nyoyo zilizojaa hasira takatifu ya kimapinduzi. Wamejitokeza uwanjani ili kumfahamisha Trump mhalifu na mnyanyasaji wa watoto, pamoja na Netanyahu mwovu na muuaji wa watoto, kwamba hawawezi kufanya lolote.
Wageni maalumu wa watengeneza historia
Maandamano ya kuvunja nguvu za maadui ya Siku ya Qudsi mwaka huu katika chimbuko la Mapinduzi ya Kiislamu pia yana wageni maalumu; leo miili mitakatifu ya mashahidi watano wapendwa wa Vita vya Ramadhani na uhalifu wa Marekani pamoja na utawala wa Kizayuni inabebwa juu ya mikono ya watu wenye shukrani wa mji mama wa ulimwengu wa Kiislamu na kusindikizwa hadi kwenye milango ya Pepo. Uwepo wa mashahidi hawa wapendwa umeyapa matembezi haya hali ya kipekee na kuwafanya watu wawe na azma kubwa zaidi ya kudai damu ya Imam wao na ya hawa waliotoa maisha yao kwa ajili ya Umma, huku hasira yao ya kimapinduzi ikionekana wazi zaidi.
Tofauti moja maalumu
Matembezi ya mwaka huu pia yana tofauti nyingine maalumu; ingawa watu wako katika huzuni kwa shahada ya Walii wa Amri wao, makamanda mashahidi na mashahidi wengine wanyonge, bado wamejitokeza uwanjani kwa hamasa na ari ya kimapinduzi ili kutoa kiapo cha utii kwa Walii wa Amri wa Waislamu, Imam wa Umma, Ayatullah Sayyid Mujtaba Khamenei mpendwa, kwa moyo wao wote, na kuitangazia dunia kwamba, wako tayari hata kutoa maisha yao kwa ajili ya Walii wa Amri wao.
Leo mji wa Qum, kama ilivyo katika nchi yetu yote pendwa, umegeuka kuwa uwanja wa maonesho ya kuvutia ya “umoja mtakatifu”. Unapoutazama umati wa watu, unaona watu wa kila tabaka, kila rangi na kila kabila, pamoja na mitazamo na mielekeo tofauti ya kisiasa, wote wakiwa wamejitokeza uwanjani. Hata wasiokuwa Wairani wapo pia.
Wananchi waaminifu wamekuja uwanjani pamoja na familia zao
Maoni yako