Ijumaa 6 Machi 2026 - 00:30
Maulama wa Najafu wahudhuria kwenye Maktaba ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Irani kwa ajili ya kutoa pole

Hawza/ Kundi la wanazuoni wa Kihindi waliopo katika hawza ya Najafu Ashraf, kwa kuhudhuria katika Maktaba ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, wameonesha huzuni zao na kutoa salamu za rambirambi, huku wakiashira kwa msisitizo nafasi yake katika upande wa elimu, dini na uongozi.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Kundi la wanazuoni wa Kihindi waliopo katika hawza ya Najafu Ashraf, kwa kuhudhuria katika Maktaba ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, kutokana na kupata kwake Shahada, wamedhihirisha huzuni zao za ndani.

Katika kikao hicho, wanafunzi wa Kihindi huku wakiheshimu huduma ya kielimu, Mapinduzi na basira ya Kiongozi Mtukufu, wameelezea kwamba; yeye ni kikngozi wa umma wa Kiislamu, hasa hasa hakurejea nyuma kwenye suala la kuwakingia kifua waliodhulumiwa na wenye kutakabari ulimwenguni, na shahada ya Kiongozi huyu Mtukufu, ni pengo kubwa kwa umma wa Kiislamu. Ujumbe na njia yake ya muqawama itabakia milele, , wanazuoni hao vile vile wamechukua kiaga juu ya kuendeleza njia na mafundisho ya Kiongozi Shahidi, katika kuwaamsha waislamu na kudumisha umoja katika umma wa Kiislamu.

Mwisho wa hafla hiyo walisoma dua kumuombea Shahidi Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ili Mwenyezi Mungu ampe daraja iliyo yajuu, na vilevile umma wa Kiislamu auunganishe na kuupa ushindi.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha