Kwa mujibu wa mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Sayyid Muhammad Saeedi katika khutba za Swala ya Ijumaa za tarehe 8 Esfand 1404 zilizofanyika katika Muswala wa Quds, Qom, huku akirejelea matukio yaliyopangwa na adui na kutokea katika vyuo vikuu, alisema: Katika vyuo vikuu kulitokea matukio machungu ikiwemo kuchomwa bendera ya Jamhuri ya Kiislamu, kuvunjiwa heshima wanafunzi wanaoswali na kutoa matusi na kejeli. Baadhi ya kauli mbiu zilizokuwa nje ya misingi ya kitamaduni ya taifa la Iran na mbali na hadhi ya wanafunzi Waislamu zilitolewa, ambazo zilikuwa sambamba na malengo ya utawala wa Kizayuni na Marekani.
Aliendelea kusema: Matendo haya maovu na ya kishetani yalionesha kwamba adui baada ya kushindwa mara kwa mara bado anajaribu kuifanya hali ya nchi isiwe salama na iwe ya taharuki ili afikie malengo yake maovu.
Mjumbe wa Baraza la Wataalamu wa Uongozi aliongeza kuwa: Mazingira ya chuo kikuu ni matakatifu. Wanafunzi wanaweza sambamba na masomo na utafiti kufanya vikao vya ukosoaji kwa ajili ya kuondoa matatizo na kuleta maendeleo nchini. Matusi na uchochezi wa moto havisaidii kurekebisha mambo ya nchi bali huleta pigo kubwa kwa heshima na hadhi ya chuo kikuu.
Akiwaelekea maadui wenye tamaa na vibaraka wao wa ndani alisema: Maadui wajue kwamba kila mpango na njama watakayokuwa nayo dhidi ya umma wa Waislamu, kwa uwepo wa wakati muafaka, umakini na uelewa wa kina wa wanachuo halisi na wa mapinduzi, watakabiliwa na kushindwa vibaya.
Msimamizi wa Haram Tukufu ya Bibi Maasuma (as) akiihutubia dola ya Marekani na utawala haramu wenye tamaa kwa vijana na wanafunzi alisema: Umma wetu wa Kiislamu umejifunza masomo na mafunzo yake kutoka katika Qur’ani. Qur’ani Tukufu kuhusu wanaovunja haki za Waislamu katika Aya ya 82 ya Suratul-Ghafir inasema:
«أَفَلَمْ یَسِیرُوا فِی الْأَرْضِ فَیَنْظُرُوا کَیْفَ کَانَ عَاقِبَةُ الَّذِینَ مِنْ قَبْلِهِمْ کَانُوا أَکْثَرَ مِنْهُمْ وَأَشَدَّ قُوَّةً وَآثَارًا فِی الْأَرْضِ فَمَا أَغْنَیٰ عَنْهُمْ مَا کَانُوا یَکْسِبُونَ؛
Je, hawakusafiri katika ardhi wakatafakari wakaona ulikuwaje mwisho wa waliokuwa kabla yao? Walikuwa wengi zaidi yao, wenye nguvu zaidi na wenye athari za kudumu zaidi katika ardhi; lakini wingi wao, nguvu zao na yale waliyokuwa wakiyachuma hayakuweza kuwaondolea chochote katika adhabu ya Mwenyezi Mungu.
Mwakilishi wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi Qom aliongeza: Enyi Wamarekani, je, mmesahau tufani ya Tabas, jinsi askari wa Mwenyezi Mungu yaani mchanga wa Tabas ulivyoharibu juhudi zenu zote na kuwaletea fedheha ya udhalilifu? Mwenyezi Mungu Mshindi bado yupo na yuko akiwavizia.
Katika sehemu nyingine ya hotuba yake akirejelea maadhimisho ya kuzaliwa Imam Hassan Mujtaba alisema: Imam Hasan (as) alizaliwa tarehe 15 Ramadhani mwaka wa tatu Hijria. Huu haukuwa uzazi wa kawaida bali ilikuwa ni nukta muhimu katika historia ya Uislamu. Imam Mujtaba (as) alikuwa mtu anayefanana zaidi na Mtume (saww).
Khatibu wa Ijumaa wa Qom aliendelea kisema: Mtume wa Uislamu sawwS) alikuwa akiwaheshimu sana Imam Hussein na Imam Hasan (as), na jambo hili katika jamii ya wakati huo, hasa kwa matukio yatakayokuja baadaye, lilikuwa na umuhimu mkubwa. Mtume (saww) alisema:
«مَن أحَبَّ الحسنَ والحسینَ فقد أحبَّنی، و مَن أبْغَضَهُما فَقد أبْغَضَنی؛
Yeyote atakayempenda Hasan na Hussein amenipenda mimi, na yeyote atakayewachukia amenichukia mimi.
Akiendelea akirejelea mwaka wa kumbukumbu ya kufariki kwa Bibi Khadija (sa) alisema: Bibi Khadija ni mfano wa mwanamke Muislamu katika kiwango cha Kiislamu, aliyekuwa na maisha ya kibinadamu, ya kiakili na ya usafi wa heshima katika jamii mbaya zaidi yaani zama za ujahilia. Katika zama ambazo mwanamke alidhalilishwa na kunyonywa kwa kiwango kikubwa. Bibi Khadija katika zama hizo alikuwa mtu mwadilifu, mwenye kuwapenda watu na mwenye akili ya kuzingatia maisha ya dunia na akhera. Alikuwa mke mpendwa zaidi kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) na mama bora kwa Bibi Zahraa (as). Fadhila nyingi alizokuwa nazo zimemfanya kuwa sura ya kuvuka nyakati na yenye kudumu.
Ayatullah Saeedi katika khutba ya kwanza alisema kiwa: Imam Hassan (as) anasema:
«فَاتَّقُوا اللَّهَ عِبَادَ اللَّهِ وَ اعْلَمُوا أَنَّهُ مَنْ یَتَّقِ اللَّهَ یَجْعَلْ لَهُ مَخْرَجاً مِنَ الْفِتَنِ وَ یُسَدِّدْهُ فِی أَمْرِهِ وَ یُهَیِّئْ لَهُ رُشْدَهُ
Enyi waja wa Mwenyezi Mungu, mcheni Mungu na mjue kwamba yeyote anayemcha Mungu, Mwenyezi Mungu humtolea njia nzuri ya kutoka katika fitna na mitihani, humfanikisha katika mambo yake na humtayarishia njia ya uongofu.
Aliendelea katika tafsiri ya Suratul-Fath akisema: Mwenyezi Mungu katika Aya ya 15 ya Suratul-Fath anasema:
«سَیَقُولُ الْمُخَلَّفُونَ إِذَا انْطَلَقْتُمْ إِلَیٰ مَغَانِمَ لِتَأْخُذُوهَا ذَرُونَا نَتَّبِعْکُمْ؛
Watasema waliobaki nyuma mtakapoondoka kwenda kuchukua ngawira: Tuacheni nasi tuwafuate.»
Imamu wa Ijumaa wa Qom alifafanua: Wale waliokhalifu na kuacha kushiriki vita vya Hudaibiyya, walipokuwa Waislamu wanaelekea katika vita vya Khaybar walitangaza utayari wao. Mwenyezi Mungu anafichua mpango wao na kusema:
«یُرِیدُونَ أَنْ یُبَدِّلُوا کَلَامَ اللَّهِ؛
Wanataka kubadilisha neno la Mwenyezi Mungu.
Alisema: Qur’ani Tukufu si kitabu kinachosimulia tu matukio ya zamani na masuala ya kihistoria; bali ni ramani ya maisha ya mwanadamu, na aya zake hung’aa kama taa ya uongofu katika njia ya mwanadamu. Qur’ani ni mwongozo bora kwa wanaotafuta ukweli.
Msimamizi wa Haram Tukufu ya Bibi Ma’suma (as) huku akieleza kwamba Aya ya 15 ya Suratul-Fath inaonesha tofauti kati ya dhahiri na batini na mpaka kati ya imani ya kweli na imani ya uongo na ya fursa, alisema: Suratul-Fath iliteremshwa mwaka wa 16 wa Utume baada ya kusitishwa vita na suluhu ya Hudaibiyya. Wakati ambapo Waislamu wa kweli walibaki katika mazingira magumu na hatari pembeni ya Mtume (saww) na wakafanya bay’a (kiaga) upya kwamba watakuwa pamoja naye hadi mwisho wa maisha; lakini kulikuwa na kundi lililorudi nyuma katika kisa cha suluhu.
Aliendelea kuwa: Mwenyezi Mungu katika sura hii amewapa Waumini wa kweli ahadi ya ushindi. Sura hii inakumbusha kwamba; watu waliokhalifu wanapoona dalili ya ngawira, mali ya dunia na ushindi huonesha vipi msimamo wao. Mwenyezi Mungu anatabiri kwamba; watu wale wale ambao katika siku ngumu hawakuambatana na Waislamu, watakapoona msafara unaelekea Khaybar watatangaza utayari wao.
Khatibu wa Ijumaa wa Qom aliongeza: Kwa mtazamo wa kwanza, utayari huu ni jambo rahisi na huenda wakaonekana wanataka kufidia; lakini Mwenyezi Mungu anafichua siri kubwa kwamba hawataki kutubia na kufidia yaliyopita, bali wanataka kubadilisha neno la Mwenyezi Mungu: «یُرِیدُونَ أَنْ یُبَدِّلُوا کَلَامَ اللَّهِ».
Alisema: Maisha ni kama shule ambayo mitihani yake wakati mwingine huja kwa shida na wakati mwingine kwa wepesi. Baadhi hudhani mitihani ya Mwenyezi Mungu ipo tu katika maradhi na vita; lakini Aya ya 15 inafundisha kwamba mtihani wa Mwenyezi Mungu unaweza kuwa katika sura ya ngawira, ushindi na kupata mali ya dunia. Wakati mwingine mafanikio na ushindi ni kioo kilicho wazi zaidi cha kuonesha sura halisi ya watu.
Mwakilishi wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi Qom aliongeza kuwa: Kwa waliokhalifu, radhi ya Mwenyezi Mungu, jihadi katika njia ya Mungu na ahadi ya uaminifu kwa Mtume (saww) si muhimu; bali kupata ngawira tu ndio muhimu. Hapa ndipo aina ya imani yao inadhihirika. Imani yenye rangi ya kimada, mara tu inapoona dalili ya fedha na cheo huamka. Hii si imani bali ni biashara waliyoingia.
Imamu wa Ijumaa wa Qom alisema: Ngawira za Khaybar kwa mujibu wa uadilifu na hekima ya Mwenyezi Mungu zilikuwa kwa wale waliokuwepo katika tukio gumu la Hudaibiyya; lakini waliokhalifu walitaka kubadilisha neno la Mungu. Tunapaswa kunyenyekea mbele ya hukumu ya Mwenyezi Mungu na kubadilisha matakwa yetu kwa hukumu ya Mungu.
Alisema: Waliokengeuka mwishoni mwa aya walitumia mbinu ya kulaumu wengine, na Mtume (saww) kwa amri ya Mungu alipokataa kwa uthabiti matakwa yao yasiyo sahihi, alisema:
«قُلْ لَنْ تَتَّبِعُونَا کَذَٰلِکُمْ قَالَ اللَّهُ مِنْ قَبْلُ فَسَیَقُولُونَ بَلْ تَحْسُدُونَنَا؛
Sema: Hamtatufuata kamwe; hivi ndivyo Mwenyezi Mungu alivyosema kabla. Lakini watasema: Bali mnatuonea wivu.
Khatibu wa Ijumaa wa Qom alisisitiza: Hapa saikolojia ya Qur’ani inasema; waliokhalifu wana tabia ya ajabu; wanapofungiwa njia badala ya kutahadhari huwasingizia wengine, na kwa kuwa wao ni wenye tamaa na wivu, hudhani wengine pia ni kama wao.
Alisema: Mwenyezi Mungu mwishoni anasema:
«بَلْ کَانُوا لَا یَفْقَهُونَ إِلَّا قَلِیلًا؛
Bali hawafahamu isipokuwa kidogo.
Upenda dunia hupofusha macho ya mwanadamu, hawezi kuelewa maana ya jihadi na kushikamana na ahadi na bay’a, na ufahamu wao hubaki katika hesabu za kimada za dunia.
Mwakilishi wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi Qom alikumbusha kuwa: Aya hii ina mafunzo makubwa kwenye kuisimamia jamii na familia. Kama wangeruhusiwa hawa wenye fursa kushiriki vita vya Khaybar, kwanza kungekuwa na dhuluma kwa wapiganaji wa kweli waliokuwepo katika tukio gumu la Hudaibiyya, kwani waliokengeuka wangepata ngawira sambamba na Waumini na kusingekuwa na tofauti kati ya mkosaji na Muumini. Pili, kungejengeka utamaduni mbaya katika jamii kwamba unaweza kukimbia siku za shida na kujitokeza wakati wa mavuno.
Ayatullah Saeedi alisema: Uthabiti huu wa Kimungu na wa Mtume (saww) katika aya hii unatufundisha kwamba; katika taasisi za kifamilia na kijamii hatupaswi kuweka sawa nafasi ya mchapakazi wa kweli na mtaka fursa, wala kuwapa malipo sawa; hata hivyo, mlango wa toba uko wazi daima, na Mwenyezi Mungu anawaahidi pia hawa waliokhalifu kwamba iwapo katika vita vitakavyokuja wataonesha imani yao kwa usahihi, watapata malipo na ujira wa Mwenyezi Mungu.
Maoni yako