Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Majina ya wabunge hao ni Ilhan Omar na Rashida Tlaib. Ilhan Omar alizaliwa Somalia lakini amekuwa raia wa Marekani kwa zaidi ya miaka 30. Rashida Tlaib ni Mmarekani mwenye asili ya Kipalestina kutoka Detroit, jimbo la Michigan, na amekuwa raia wa Marekani maisha yake yote.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wawili hao pamoja na wabunge wengine walipaza sauti wakati wa hotuba ya Trump wakipinga sera zake, hususan kuhusiana na masuala ya uhamishaji wa wanajeshi katika maeneo ya vita. Waliripotiwa kupaza sauti wakisema: “Umewaangamiza Wamarekani!”
Inadaiwa kuwa Trump alitoa amri ya kuwaondoa katika ukumbi wakati wa hotuba yake, na kabla ya kutoka kabisa, wabunge hao waliripotiwa kupaza sauti tena kauli hiyo wakiwa karibu na mlango wa kutokea.
Aidha, Trump alifanya mashambulizi ya kisiasa dhidi ya msanii maarufu wa Marekani Robert De Niro, mshindi wa tuzo mbili za Academy Awards (Oscar), akimtaja kwa maneno makali kutokana na kuwa miongoni mwa wakosoaji wake wakubwa wa kisiasa.
Chanzo: Middle East Monitor
Maoni yako