Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha SShirika la Habari la Hawza, kwa kunukuu tovuti rasmi ya haram hiyo, katika maonyesho haya kazi mbalimbali za sanaa zimewasilishwa, zikiwemo uchoraji, michoro ya kisasa na ya kale, sanaa ya kidijitali, pamoja na nakala za maandishi ya kale zenye thamani kubwa. Dhamira ya mkusanyiko huu ni kuonyesha umoja wa kauli kati ya lugha na tamaduni mbalimbali duniani, pamoja na kuleta ukaribu wa mitazamo ya watu wa dunia kuhusu kusubiri faraja ya Imam Mahdi (a.f.).
Sayyid Kazem al-Khurrasan, mkurugenzi wa Kituo cha Masomo Maalumu ya Imam Hasan (a.s.), alielezea maonyesho haya kuwa yanaakisi ujumbe wa kuunganisha unaovuka mipaka, na yanawasilisha dhana ya kusubiri faraja kwa wokovu kama thamani ya pamoja ya kiroho na kibinadamu kwa wageni wanaotembelea.
Dkt. Abdulhadi al-Ibrahimi, mkuu wa kitengo cha mabaki ya kale na urithi wa kitamaduni, alisisitiza nafasi ya sanaa katika kuimarisha mazungumzo kati ya tamaduni mbalimbali na akasifu athari ya dini katika kuwaongoza wasanii kuelekea maana ya kina zaidi. Aliongeza kuwa tukio hili ni sura ya kimataifa ya sanaa ya Kiislamu na linaimarisha mwingiliano wa kimataifa.
Rais wa Taasisi ya Sanaa na Vyombo vya Habari ya Qaaf, pia katika mahojiano alisema: Wasanii wanaoshiriki wanawakilisha nchi na madhehebu mbalimbali kama mabalozi wa kitamaduni wa mataifa yao. Washiriki kadhaa kutoka nchi kama China na Brazil wanaitembelea Iraq na Najaf kwa mara ya kwanza, jambo linaloongeza upana wa mahusiano ya kimataifa na ujumbe wa jumla wa maonyesho haya.
Tukio hili limewakutanisha wasanii 60 kutoka nchi 14 duniani ili kuakisi tamaduni na mila mbalimbali.
Chanzo: Karbala Now Agency
Maoni yako