Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah A‘raafi, Mkurugenzi wa Hawza, alikutana na kufanya mazungumzo na Mtukufu Ayatullah Nouri Hamedani, na akawasilisha ripoti ya mipango na shughuli kuu za Hawza.
Katika mkutano huo, Mtukufu Ayatullah Nouri Hamedani, akielezea huduma zenye thamani kubwa za Ayatullah A‘raafi katika uongozi wa Hawza, alitoa pongezi zake kutokana na kuandaliwa kongamano la kumuadhimisha Ayatullah Mirzaay Naa’iniy — radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.
Mtukufu huyo pia alitaja hotuba ya Ayatullah A‘raafi aliyotoa huko Najafu Ashraf kuwa ni hatua inayostahiki katika kuitambulisha nafasi ya kielimu na kifiqhi ya Ayatullah Mirzaay Naa’iniy — radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.
Maoni yako